MVUA YAACHA KILIO TANGA
maguruacademy Thursday, December 20, 2018 Nyumba zaidi ya 300 zimezama na maji baada ya kukumbwa na mafuriko katika Kata ya Magaoni, hivyo kusababisha wakazi wake kuhama makazi yao. Tukio lilo lilitokea usiku wa kuamkia jana majira ya saa 7:00 usiku
baada ya mvua kubwa kunyesha usiku kucha. Mwenyekiti wa Kata ya Magaoni, Kassim Abdallah, ambaye pia nyumba yake
imezama, alisema kuwa mvua iliyonyesha usiku wakuamkia jana,
imeacha hasara kubwa kwa wakazi wa kata hiyo kutokana na kuzingirwa na maji, huku mali mbalimbali zikiharibika.
Alisema mvua hiyo ilianza kunyesha wakati huo mpaka saa 2:00 asubuhi, hivyo kusababisha idadi kubwa ya wananchi kukosa mahali pa kuishi, hivyo kuhamia katika shule na wengine kuhifadhiwa kwa ndugu na jamaa zao.
Abdallah alisema kata hiyo ni mpya kwa kuwa mwanzo ilikuwa sehemu ya kata ya Mabawa kabla ya kugawanywa. Alisema sababu kubwa ya mafuriko hayo ni kukosekana kwa mifereji ya kutosha, hivyo kushindwa kuruhusu ma...