Posts

Showing posts from December 18, 2018

Mourinho anaondoka Man United :AKUMBUKWA KWA REKODI HII

Image
Club ya Man United imetangaza kumfuta kazi aliyekuwa kocha wake mkuu mreno Jose Mourinho kutokana na mwenendo mbovu wa timu hiyo ambao umekuwa ukienda kwa kusuasua msimu huu, uongozi umeamua kumfuta kazi Jose Mourinho na kumtangaza Michael Carrick ambao ni mchezaji wao wa zamani kuwa kocha wa muda wa timu hiyo. Jose Mourinho anafutwa kazi ikiwa ni miaka miwili imepita tokea aajiriwe kuwa kocha wa timu hiyo mwaka 2016, moja kati ya tukio kubwa linalochukua headlines kuhusu Jose Mourinho ni kuhusiana na kufanana kidogo tarehe ya leo December 18 2018 kufutwa kazi Man United inataka kufanana na siku ya December 17 2015 aliyofutwa kazi na Chelsea zikiwa zimepishana siku moja. Hadi sasa Man United wapo nafasi ya 6 katika msimamo wa Ligi Kuu England msimu huu, wakicheza michezo 17, sare michezo mitano, ushindi michezo 7 na wamepoteza michezo mitano wakiwa na point 34, hata hivyo Mourinho anaondoka Man United akiwa atakumbukwa kwa rekodi ya ki

Mourinho: aendelea kuharibiwa

Image
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amekuwa ni mwiba kwa kocha Jose Mourinho baada ya kufutwa kazi Man United na hii nikutokana na rekodi zilizopita. Ikumbukwe kuwa mnamo Aprili, 2013, Mwezi mmoja baada ya kipigo cha mabao 4-1 kutoka kwa Dortmund chini ya Jurgen Klopp, Mourinho akatimuliwa Real Madrid. Miaka miwili baadaye Chelsea ikamtimua Mourinho baada ya kufungwa mabao 3-1 na Liverpool pale Stamford Bridge. Sasa Klopp kaiongoza tena Liverpool kuitwanga Man United 3-1 na Mourinho kafutwa kazi!

TAMKO :vyama vya Upinzani kuhusu Zanzibar

Image
Na.Thabit Madai,Zanzibar Vyama sita vya upinzani vilivyokaa kikao chao Zanzibar vimesema mwaka wa 2019 ni mwaka ambao  watapambana kwa hali zote katika kudai haki zao wanazonyimwa kinyume na sheria za Serikali ya Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania. Kauli hiyo ilitolewa na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Maalim Seif Shariff Hamad wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza kikao hicho cha siku tatu kilichofanyika Zanzibar kwa niaba ya vyama hivyo. "Kama vyama vya siasa  vyenye uhalali na uratibu wa  uliowekwa rasmin kikatiba, tunatangaza rasimi namna ya kufanya mikutano yetu ya hadhara katika kila kona ya nchi yetu’’ alieleza Maalim Seif. Alieleza hawatoruhusu katazo haramu ambalo alisema linakwenda kinyume na sheria za nchi na kudai haliwezi kuzuia kazi zao.  Aliwataka wanachi pamoja wanachama wote wa vyama sita, wakati ni sasa wa kuondoa hofu na kuunga mkono vyama vyao ili kulinda Demokrasia.  "Hatupaswi kuwa waoga hata kidogona hatup

MAGAZETI YA LEO 19/12/2018

Image

Waziri wa Viwanda atoa siku 14 Brela

Image
Nora Damian, Dar es Salaam Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Joseph Kakunda, ametoa siku 14 kwa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), kurekebisha mifumo ya kielektroniki ya utoaji huduma za wakala huo. Akizungumza baada ya kutembelea wakala huo leo Desemba 18, Kakunda amesema mifumo ya kielektroniki imekuwa ikilalamikiwa na watu wengi hasa katika siku za karibuni. “Ndani ya wiki mbili nimekuja tena hapa kwa sababu kuna sababu maalumu, udhaifu mkubwa uko kwenye mifumo kuliko uhalisia. “Kila nikipokea simu 10 za wafanyabiashara nane zinalalamikia Brela hili ni tatizo,” amesema Kakunda. Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Brela, Emmanuel Kakwezi, amesema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali kama za upungufu wa watumishi 51 na mfumo kutokuwa imara. “Kuna changamoto ya mtandao wa ORS katikati yakazi unaweza kuzimika. Mteja anatuma maombi lakini haionekani na sisi tunaweza kumjibu lakini haoni,” amesema Kakwezi.

Haswa :CCM yazidi kujiimarisha

Image
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimemrejeshea uanachama wa chama hicho aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dares Salaam, Ramadhani Madabida na wenyeviti wengine wanne baada ya kujiridhisha na maombi yao ya kutaka kusamehewa kwa makosa yao wakiwa wenyeviti wa chama hicho. Aidha, halmashauri hiyo, imemuweka chini ya uangalizi aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu, ambaye pia ameomba kurejeshewa uanachama baada ya kufukuzwa kwa makosa ya kimaadili. Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Jumanne Desemba 18, Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally, amewataja waliosamehewa pamoja na Madabida ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Shinyanga, Erasto Kwirasa, Christopher Sanya (Mara) na aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge. “Hatua hiyo imefikiwa leo katika kikao cha halmashauri ya chama  kilichoongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli ambapo pamoja na mambo me

Zitto ni mchawi, kaniroga sana kashindwa na sio raia wa Tanzania- Katibu UVCCM Kigoma

       Zitto ni mchawi, kaniroga sana kashindwa na sio raia wa Tanzania- Katibu UVCCM Kigoma Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Kigoma, Agustino Matefu amepokea zaidi ya wanachama 100 kutoka chama cha ACT-Wazalendo. Katika mkutano huo wa kuwapokea wanachama hao uliofanyika jijini Dar es salaam, wanachama hao wakiwemo madiwani wamesema kuwa, wameamua kukihama chama hicho baada ya kuona kinakosa muelekeo. “Kama mnavyoona waandishi wa habari, hawa wote siwajui lakini wameamua kuniita ili waweze kujiunga na chama cha mapinduzi CCM, na hizi ni salamu kwa Zitto kwamba 2020 atafute kazi ya kufanya au arudi kwao Kongo,”amesema Matefu.

Viongozi wa upinzani wafanya kikao cha siri Zanzibar

Image
Viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani nchini wamejichimbia visiwani Zanzibar kwa ajili ya kupatiana mafunzo mbalimbali juu ya mwenendo wa siasa na demokrasia. Viongozi waliohudhuria ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamadi, pamoja na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa na Kiongozi wa ACT – Wazalendo Zitto Kabwe. Mbali na hao, viongozi wengine walionekana na Rais wa Chama Cha Mawakili Tanzania, (TLS) Fatma Karume pamoja viongozi wengine mashuhuri nchini ambapo imeelezwa walijadili juu ya mwenendo wa hali ya kisiasa nchini. Aidha, Kaimu Msemaji wa chama cha CUF, Mbarara Maharagande amesema kuwa kikao hicho kimeandaliwa na taasisi ya Marekani IR kupitia kwa Katibu wa CUF, Maalim Seif. “Ni kweli kuna semina inafanyika ya viongozi wa vyama inafanyika Zanzibar ambayo inafanyika kwa siku tatu, na aliyewaalika ni Katibu Mkuu wetu Maalim Seif na imeandaliwa na taasisi ya IRSA, watu wa democratic ya America,” amesema Maharagande.

Sababu nane za kufutwa safari za Fastjet

Image
MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imetaja sababu nane za kufuta safari za ndege za Shirika la Fastjet Tanzania na kuipa notisi ya siku 28 kujieleza kwanini wasifutiwe leseni ya kuendesha biashara hiyo nchini. Wakati TCAA ikieleza hayo, Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha, ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika hilo na mwanahisa mkubwa wa Fastjet Tanzania, alipotafutwa kuzungumzia hali hiyo alisema yupo kwenye kikao. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari, alitaja sababu hizo kuwa ni kutokuwa na ndege baada ya moja kati ya mbili zilizosajiliwa nchini kuharibika na kupelekwa nje ya nchi kwa matengenezo, huku moja ikizuiwa na mamlaka hiyo. Ndege hiyo ilizuiwa baada ya kampuni iliyowakodishia Fastjet kuitaka irudishwe kwa kile walichodai kuwa inafanya kazi bila wao kupata chochote. Alisema kutokana na uamuzi huo wa mkodishaji kutaka arejeshewe ndege yake, alilazimika kuizuia kama am

TMA yatoa tahadhari mafuriko yaja

Image
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) imetoa tahadhari ya kuwepo kwa mvua kubwa zitakazosababisha mafuriko katika baadhi ya mikoa nchini kwa muda wa siku tano. Taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo leo Jumanne Desemba 18, imeitaja mikoa ambayo leo itakuwa na mvua kubwa ni Njombe, Ruvuma na Morogoro Kusini na kesho Jumatano Desemba 19 maeneo yanayotarajiwa kuwa na mvua ni Rukwa, Mbeya, Songwe, Njombe, Iringa, Ruvuma, Dodoma, Singida, Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga, Pwani, Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, Ruvuma,Morogoro, Unguja na Pemba. “Kuanzia Jumatatu Desemba 17 hadi Ijumaa Desemba21 kutakuwa na mvua kubwa ambazo zitasababisha maji kujaa na kupita kwa kasi jambo ambalo ni hatari kwa maisha ya watu. “Hivyo, mamlaka inatoa tahadhari kuwa mvua hiyo itakayoambatana na upepo na kusababisha msongamano wa magari na watu na hivyo kuchelewesha usafirishaji hasa katika maeneo ya mijini hivyo watu wa maeneo hayo wanapaswa kuchukua tahadhari zitakazoachwa na mvua

Serikali yashtukia udanganyifu bima ya afya

Image
SERIKALI imeonya watu wanaojihusisha na vitendo vya udanganyifu katika sekta ya Bima ya Afya nchini ikisema  watakaobainika watakuwa wametenda kosa la jinai. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile alikuwa akizungumza katika mkutano ulioandaliwa na Umoja wa Kampuni za Bima ya Afya Tanzania (ATI) Dar es Salaam jana. Alisema Serikali inatambua  udanganyifu huo hufanywa na baadhi ya watoa huduma za afya na watu wanaotibiwa kwa mfumo huo. Wakati mwingine vitendo hivyo hufanywa kwa ushirikiano kati ya wafanyakazi wasio waaminifu pamoja na wateja, alisema. Dk. Ndugulile alionya kuwa wanaojihusisha na udanganyifu huo kwenye huduma za Bima ya Afya  wanatenda kosa la jinai na adhabu yake ni kifungo   na faini. “Serikali ya awamu ya tano inapinga kwa vitendo rushwa na udanganyifu na yeyote anayejihusisha na vitendo hivyo huchukuliwa hatua kali za  sheria. Serikali hii imeelekeza nguvu zake katika kujenga mfumo na taifa

JPM alivyomsifia Mufti wa Tanzania

Image
Anna Potinus – Dar es salaam Rais John Magufuli amempongeza Shekhe Mkuu na Mufti wa Tanzani, Aboubakar Zubeir kwa kazi nzuri aliyoifanya katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake huku akidai ni mtu wa tofauti katika utendaji kazi wake. Pongezi hizo amezitoa leo Desemba 17, 2018 katika maadhimisho ya kilele cha miaka 50 ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) jijini Dar es

Waziri Mkuu Majaliwa ampongeza, Mufti amtaka amalize migogoro yote

Image
Bethsheba Wambura, Dar es Salaam Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kwa kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania, Sheikh Aboubakary Zuberi migogoro ya misikiti imepungua. Licha ya kupungua huko Waziri Majaliwa amemtaka Sheikh huyo aongeze bidii, ubunifu na kasi kubwa ili afanikishekumaliza migogoro yote inayokabili misikiti nchini. Akizungumzia umuhimu wa dini Waziri Majaliwa amesema uwepo wa dini mbalimbali nchini ni muhimu  kwa kuwa umesaidia kuunga mkono jitihada mbalimbali za serikali katika kuhakikisha nchi inasonga mbele. Waziri Mkuu amesema hayo leo Desemba 17, jijii Dar es Salaam katika maadhimisho ya miaka 50 tangu kuaanzishwa kwa Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata). Amesema kila dini kwa imani zao wanasaidia kutekeleza mambo ambayo kikawaida yangetakiwa kufanywa na serikali. Akizungumzia sekta ya Afya amesema vituo vya kutoa huduma za afya nchini vimejengwa na taasisi za dini. “Katika elimu taasisi za d

Nafasi za Kazi 158 hizi hapa:pata ajiraleo

Image
On behalf of Tanzania Railway Corporation (TRC), The Cereals and Other Produce Board of Tanzania and Water Institute (WI) President’s Office, Public Service Recruitment Secretariat invites qualified Tanzanians to fill 158 vacant posts as mentioned below; 1.      INTRODUCTION – TANZANIA RAILWAY CORPORATION (TRC) Prior to May-2017, Tanzania owned a Railway network built more than 115 years ago by Germany and later British, along central corridor having Meter Gauge standards. The GoT through TRC is has lunched development of SGR network whereby as of to date, Feasibility Studies are completed to cover more than 4,880 route-km of SGR network in the Country, distributed in three corridors namely Central corridor which runs from Dar Port via Dodoma and Tabora to North and West parts of Tanzania reaches borders with land locked Countries of Uganda, Rwanda, Burundi, DRC and Zambia; Southern Corridor of Mtwara to Amelia Bay, within Mbamba Bay areas, with spurs to Mchuchuma and