Posts

Showing posts from 2019

TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA ZA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI

TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA ZA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI 27 February 2019 Tangazo la Ajira Tangazo_Ajira_Mpya_Walimu_Feb2019.pdf Kuomba ajira bofya hapa http://ajira.tamisemi.go.tz

Sakata la Korosho laibuka Bungeni, Serikali yatoa majibu

Image
Sakata la bei ya korosho laibuliwa bungeni mara baada ya kuwepo taarifa za kununuliwa zao hilo chini ya bei elekezi ya Tsh. 3,300 kwa kilo. Naibu Waziri wa kilimo, Omar Mgumba amesema kuwa Korosho hununuliwa kwa bei ya 3,300 kama alivyoelekeza Rais Magufuli na bei hiyo haijakiukwa. Hata hivyo ameeleza kuwa bei ya Tsh. 3,300 kwa korosha daraja la kwanza, huku daraja la pili ikinunuliwa kwa Tsh. 2,640. "Hadi kufikia January 30, 2019 Serikali imenunua jumla ya tani 214,269.684 za korosho ghafi zenye thamani ya Sh. 707,089,957,200.00 sawa na asilimia 89.3 ya lengo la uzalishaji," amesema. Aliendelea kwa kueleza kuwa jumla ya wakulima 390,466 wamekwisha lipwa  hadi kufikia January 30 mwaka huu, huku Vyama vya msingi 603 vimelipwa kati ya vyama vya msingi 605 vilivyohakikiwa. Utakumbuka awali Mbuge wa Mchinga kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Awali Bobali alisema kuwa korosho imekuwa ikinunuliwa kwa bei ya Tsh. 2,640 kwa kilo na yupo tayari kujiuzulu iwapo ni kwel

Ubelgji yakubali kumpa hifadi Gbagbo

Image
BLUSSELS,Ubelgji SERIKALI ya hapa imekubali kumpa hifadhi kiongozi wa zamani wa Ivory  Coast, Laurent Gbagbo, wakati akisubiri matokeo ya rufaa iliyokatwa kupinga kuachiwa na Mahakama ya Kimataifa inayoshughulikia Makosa ya Uhalifu wa Kivita ICC iliyopo mjini  The Hague nchini Uholanzi. Hatua hiyo imekuja baada ya Januari 15 mwaka huu Mahakama hiyo kumwachia  Gbagbo na msaidizi wake,  Charles Ble Goude,baada ya kuwafutia mashtaka ya kuhusika na ghasia zilizolipuka katika taifa hilo la magharibi mwa Afrika mwaka  2010. Baada ya kufikia uamuzi huo, kesho yake mahakama hiyo ikaeleza kuwa haioni sababu ya kuendelea kumshikilia mahabusu na hivyo ikasema kuwa inaweza kumkabidhi kwa nchi ambayo itakuwa tayari kumpokea. “Kulikuwa na ombi kutoka mahakamani la kumpa hifadhi  Gbagbo na hiyo ilikuwa kazi rahisi kwa sababu ana familia nchini Ubelgji kwani mkewe na wanawe wanaishi Brussels,” Waziri wa Mambo ya Nje wa hapa,  Didier Reynders alikiambia kituo cha televisheni ya umm

AJALI:magari yagongana pia kuwaka moto kusababisha vifo vya waili

Image
(Picha siyo ya tukio lenyewe)  Watu wawili wamefariki papo hapo na wengine wawili kujeruhiwa baada ya magari mawili kugongana uso kwa uso kisha kuwaka Moto mkoni Morogoro. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa amesema kuwa ajali hiyo imetokea katika eneo la Makunganya Mkoani mkoani humo majira ya saa 11 alfajiri. Majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa hospitali ya mkoa wa Morogoro ambapo inaelezwa kuwa mmoja wapo hali yake ya kiafya kuwa mbaya zaidi.

Mahakama ya DR Congo yaidhinisha ushindi wa Felix Tshisekedi, Fayulu aitisha maandamano

Image
Mahakama ya katiba DR Congo imemuidhinisha rasmi Felix Tshisekedi kuwa rais wa nchi hiyo. Mgombea aliyechukua nafasi ya pili katika matokeo ya uchaguzi wa urais nchini DR Congo Martin Fayulu ameitaka jamii ya kimataifa kutotambua matokeo hayo na ameitisha maandamano. Taarifa yake inajiri baada ya ya mahakama ya kikatiba kuidhinisha ushindi wa mgombea mwengine wa upinzani , Felix Tshisekedi . Muungano wa Afrika ulisema siku ya Ijumaa kwamba kulikuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu matokeo hayo na kutaka matokeo rasmi kucheleweshwa. Bwana fayulu sio mgombea pekee ambaye anaamini kwamba yeye ni muathiriwa wa wizi wa kura huku data ilioibwa ikionyesha kuwa alipata kura mara tatu ya kura alizopata Tshisekedi. Haijulikani iwapo raia wataheshimu wito wa Fayulu wa kufanya maandamano. Siku ya Jumatatu ujumbe wa AU unatarajiwa Kinshasa na unatarajiwa kukutana na mtu anayedaiwa 'kuiba' kura rais anayeondoka madarakani Joseph Kabila. Iwapo Tshisekedi ataapishwa , muungano

Ndugai Tundu Lissu, ‘Unatakiwa urudi haraka’

Image
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amemtaka Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu kurejea nyumbani kwa kuwa hana kibali cha kuwa nje ya nchi. Ndugai amesema kuwa hawezi kumpangia Lissu mambo ya kusema ila ajue hana kibali cha kuendelea kuwa nje ya nchi wakati ofisi ya Spika haina taarifa. “Yeye ametoka kuugua aache uzushi arudi nyumbani, tunamsubiri nyumbani, kitu muhimu ni kwamba ajue hana ruhusa ya Spika ya kuwa huko anakozurura, sasa achunge kidogo, maana Spika ana nguvu zake, asimpe sababu,”amesema Ndugai. Aidha, Lissu ambaye amepona majeraha aliyopata baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 na watu wasiojulikana mwaka juzi, amedai kigezo kinachotaka kutumika kumvua ubunge ni utoro bungeni, ametoa waraka aliouita ‘Baada ya risasi kushindwa, sasa wanataka kunivua Ubunge’. Aidha, Lissu ameandika kwenye ukurasa wake wa kijamii kuwa, ”Ni taarifa gani ya maandishi watu hawa wanahitaji wakati nilishambuliwa nikiwa kwenye vikao

HABARI KUBWA LEO JUMATATU 21/1/2019

Image

CAG ashindwa kunyamaza, amjibu Spika

Image
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali (CAG), Prof. Mussa Asad amesema kuwa ameitika wito wa kisheria kutoka wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Maadili na Madaraka ya Bunge uliyomtaka kwa ajili ya mahojiano ifikapo January 21 mwaka huu.

HABARI KUBWA LEO IJUMAA 18/1/2019

Image