Posts

Showing posts from January 7, 2019

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU KUSOMA "DEGREE" BILA KUPITA "FORM SIX".

Image
Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Pro.Joyce Ndalichako amepiga marufuku wanafunzi kujiunga na masomo ya Shahada (degree) bila kupita kidato cha sita. Marufuku hiyo itaanza rasmi katika mwaka ujao wa masomo. Prof.Ndalichako emesema mfumo wa elimu huria umechangia kuzalisha wasomi butu kwa kupokea wanafunzi dhaifu kitaaluma. Ndalichako amesema wanafunzi wanaofeli kidato cha nne na kwenda kusoma certificate na baadae diploma ili wajiunge vyuo vikuu hawataruhusiwa kujiunga na masomo ya shahada (degree) kama hawajarudia (reseat) masomo yao na kupata alama za kwenda kidato cha tano, na wafanye mitihani ya kidato cha sita na kufaulu ndipo wajiunge vyuo vikuu. Katika utaratibu huo, wanafunzi wa kidato cha nne watakaoruhusiwa kusoma shahada (degree) bila kupita kidato cha 5 na 6 ni wale waliofaulu kidato cha 4 na wakachaguliwa kwenda kusoma katika vyuo vya ufundi daraja la kati (Technicians). Lakini wale wanaokosa "credit" za kuendelea form five na kuamua kwenda certificate mw

NEW ANOUNCEMENT:PRACTICALS ,PRACTICALS ,PRACTICALS

WADAU WOTE WA ELIMU MNATANGAZIWA KUWA ,NOTES ZA MASOMO YA SAYANSI KWA VITENDO (PRRACTICAL) BIOLOGY ,PHYSICS, CHEMISTRY KWA UPANDE WA OLEVEL, ZINAPATIKANA HAPA ZINGINE PIA

NEW: TIME TABLE JANUARY -2019 NOW IS OUT

Udhaifu' wa Bunge wamponza CAG na Mdee

Image
Spika wa Bunge Job Ndugai (Mb) amemtaka  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Mussa Assad  na  Mbunge wa Kawe Mhe. Halima Mdee kufika  mbele ya Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ili kujieleza kufuatia kauli za kudhalilisha Bunge. Kushoto ni CAG Prof. Mussa Assad, kulia ni Mbunge wa Kawe Halima Mdee Taarifa iliyotolewa na Mhimilili huo imesema kwamba viongozi hao wamelidhalilisa bunge kwa kuliita kuwa ni dhaifu ambapo Prof. Assad alitoa kauli hiyo akiwa nje ya nchi. Spika Ndugai ametaka Mussa Assad, CAG afike mwenyewe kwa hiyari yake mbele ya kamati ya maadili ya Bunge tarehe 21. 01.2019 vingenevyo atapelekwa kwa pingu huku Mdee akitakiwa kwenda tarehe 22. Hivi Karibuni CAG akijibu swali la  Mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa alisema kitendo cha ofisi yake kufanya ukaguzi na kutoa ripoti zenye kuonyesha kuna ubadhirifu lakini baada ya hapo wananchi hawaoni kinachoendelea ni kutokana na

Zitto awaponza viongozi wa ACT Wazalendo

Image
Jeshi la Polisi Wilayani Kigoma linawashikilia viongozi watatu wa Ngome ya Vijana Jimbo la Kigoma Mjini waliokwenda polisi kutoa taarifa ya kufanya maandamano ya amani. Zitto Kabwe Ngome hiyo ya vijana imeeleza kuwa mpaka sasa hakuna taarifa rasmi ya sababu gani polisi imewashikilia viongozi hao wa Vijana Kigoma Mjini huku ikidai kuwa huenda wakakosa kabisa dhamana kwa siku ya leo. Viongozi wanaoshikiliwa na Polisi ni Said Mlindwa (Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana Jimbo), Wakili Mubanga (Katibu wa Ngome ya Vijana Jimbo) na Ntakije Ntanena (Katibu Mwenezi wa Ngome ya Vijana Jimbo) Maandamano ambayo walikuwa wameenda kuyaombea kibali ni ya amani kwaajili ya  kumpongeza Mbunge wao Zitto Kabwe na madiwani kwa kazi wanayoifanya kuwaletea wananchi maendeleo. Aidha Ngome hiyo ya Vijana imesisitiza kuwa inawaombea dhamana kwakuwa ni haki yao na wanapaswa kupewa kwa kuwa masharti ya dhamana kwa mujibu wa sheria yametimizwa.

Wastaafu waandamana hadi NSSF kushinikiza walipwe mafao yao

Image
Bethsheba Wambura, Dar es Salaam Zaidi ya wanachama 200 wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), wamekusanyika katika Ofisi ya Mkoa wa Kinondoni wakishinikiza kulipwa mafao yao. Wastaafu hao wamekusanyika leo kuanzia saa sita mchana katika ofisi hizo Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam, ambapo wako waliostaafu kuanzia mwaka jana kurudi nyuma ambapo pamoja na mambo mengune wamedai hawajui ni kwanini hawalipwi mafao yao wakati Rais John Magufuli ametangaza wapewe mafao yao kwa wakati. Akizungumza na Mtanzania Digital mmoja wa wastaafu hao, Khamis Khamis, amesema yeye amestaafu tangu Juni mwaka 2018 lakini kila anapoenda kudai mafao yake anapigwa tarehe hali inayomfanya anashindwa kulipia watoto ada za shule ama kufungua biashara. Amesema wamekusanyika ili kupatiwa stahiki zao huku wakishinikiza kitumike kikotoo cha zamani na sio kile cha asilimia 33.3 kwani mtu anakuwa anadai fedha nyingi ila anapewa kidogo sababu tu sheria hairuhusu wakati Rais Magufuli alisema kila anayestaaf

MAGAZETI YA LEO 8/1/2019

Image
Fahamu yote yaliyojiri katika Magazeti ya Tanzania leo Januari 8, 2019. Hapa unapata habari zote zilizopewa uzito katika kurasa za mbele na kurasa za nyuma za habari za michezo na burudani.