DIAMOND AFUNGUKA BAADA YA KUOMBA RADHI BASATA, WASAFI FESTIVAL INAENDELEA
BAADA ya kufungiwa na Baraza La Sanaa Tanzania (BASATA), msanii Diamond pamoja na Rayvanny Desemba 21 mwaka huu, na baadaye kuomba radhi katika Baraza la Sanaa la taifa ‘BASATA’, tayari Diamond amelazimika kueleza makubaliano yake na baraza hilo jambo linalomfanya sasa aweze kuendelea na tamasha lake la Wasafi Festival 2018 nchini Kenya.
Akiwa nchini Kenya kwenye kikao chake na waandishi wa habari alisema, “Serikali yetu inatupa sapoti kubwa sanahivyo kilichotokea ni makosa yetu wenyewe kwani wimbo wimbo wetu wa Mwanza ni wazi ulikuwa hautakiwi kufanyiwa shoo nchini kwentu, lakini kwa sisi wasanii kama mjuavyo tunapoikua jukwaani kuna muda huwa tunakuwa na mizuka ya kupitiliza nadhani ndicho kilichotokea kwetu kiasi cha kukosea na kujikuta Serikali yetu inatuadhibu kwa kufata za Baraza letu.
“Sisi tkuiwa kama moja wa raia wema nchini kwetu, tulilazimika tuandike barua ya kuomba radhi kwa mashabiki na uma wote kwa ujumla kwa sababu tunatambua tulikosea.
“Mbali na kuomba radhi kwa umma pia tulilazimika kuomba radhi kwa barua Basata na zaidi tulizingatia kuwa tuna shoo nyingine muhimu hapa nchini Kenya.
“Kwakua Serikali yetu ni elewa na imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha inasapoti muziki na wanatupenda kama watoto wao na kwamba siku zote wamekuwa wakipenda tuendelee kufanya vitu vizuri walituruhusu na ndiyo maana tupo hapa leo,” alisema Diamond.
Mpaka muda huu, hakuna taarifa kamili kutoka BASATA kuhusiana na kutengua adhabu hiyo.
TAZAMA VIDEO HAPA
Comments