Meli zachangamsha biashara ya usafirishaji


MELI za mizigo za MV Ruvuma na MV Njombe zimeongeza mwamko wa biashara, hasa usafirishaji makaa ya mawe katika bandari za Ziwa Nyasa.
Makaa ya mawe husafirishwa kutoka Bandari ya Ndumbi wilayani Nyasa hadi katika Bandari ya Kiwira iliyopo wilayani Kyela.
Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea bandari za Itungi na Kiwira juzi, Meneja wa bandari za Ziwa Nyasa, Abed Gallus alisema meli hizo zenye uwezo wa kubeba tani 1,000 kila moja zimegharimu Sh bilioni 11 na zilianza kutengenezwa mwaka 2015 na kukamilika mwaka jana.
“Meli za mizigo na ujenzi wa meli ya abiria (MV Mbeya) ni miradi ya maendeleo tuliyoanza kuitekeleza mwaka 2015 ili kuongeza ufanisi wa bandari za Ziwa Nyasa.
“Tunashukuru mwamko wa wateja umeanza kuwa mzuri, hasa wale wanaojihusisha na biashara ya makaa ya mawe,” alisema Gallus.
Alisema meli hizo tayari zimeshafanya safari saba hadi sasa na kati ya hizo, nne zilikuwa za majaribio na tatu za kibiashara ambazo zilifanywa kati ya Septemba na Novemba mwaka huu.
Meneja huyo alisema katika kipindi hicho walisafirisha tani 2,400 za makaa ya mawe na matarajio yao ni kusafirisha tani 48,000 kwa mwaka.

Comments

Popular posts from this blog

KESI YA ZITTO MUSWADA WA SHERIA YA VYAMA VYA SIASA YAHAMISHWA

Waziri asimamisha likizo za Marubani ATCL