Tabora:Wauguzi wanaotoa lugha chafu waonywa
WAUGUZI na watoa huduma za afya wa zahanati, vituo vya afya na hospitali mkoani Tabora, wametakiwa kufuata maadili ya kazi yao na kuacha kutoa lugha chafu zenye maudhi au kebehi kwa akinamama wajawazito wanaoenda kupata huduma. Onyo hiyo, limetolewa juzi na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Tabora, Mwajuma Mhina ambaye alisema baadhi ya akinamama wakiwemo wajawazito wamekuwa wakitendewa ukatili na wauguzi kwa kutolewa lugha chafu afya jambo ambalo ni kinyume na maadili ya kazi hiyo. Alisema wauguzi kama hao hawawezi kufumbiwa macho kwa kuwa vitendo vya vinadhalilisha utu wa mwanamke na kuwaomba kutoa huduma kwa kuzingatia maadili na misingi ya kazi. “Huu ni unyanyasaji kwa akinamama, unawezaje kutoa lugha zisizofaa wakati wa mgonjwa akihitaji umuhudumie, umesomea kuwahudumia huo ndiyo wajibu wako utimize.., lakini kwa kuwa wapo wasiosikia tunaiomba Serikali kupitia wizara ya afya kufuatilia na kuwachukuliwa hatua,”alisema. Al...