Shirika la ndege la Fastjet laamua kuingiza ndege mbili

“Kuanzia Jumamosi tukakuwa na ndege mbili aina ya Boeing 737 (pamoja na iliyopo sasa) ambazo zitakuwa tayari kufanya kazi. Hii itasaidia kuondoa kero ya kusitishwa kwa safari,” amesema Masha.
“Ndege zote zitakuwa na usajili wa Tanzania na kutokana na mahitaji na msimu, hivi karibuni tunaweza kuongeza ndege nyingine moja au mbili aina ya Bombardier.”
Amesema ana imani shirika litainuka na kuwa imara zaidi na juhudi zinazofanyika sasa ni kuzungumza na mamlaka ili kuwaruhusu kuanza kuuza tiketi.
Amesema tayari baadhi ya matakwa ya mamlaka hiyo yametimizwa au kujibiwa ingawa bado mazungumzo yanaendelea.
“Tunatarajia kurejesha safari zetu za Nairobi na Afrika Kusini kuanzia Februari 2018 na kuanza kwenda Songea, Dodoma, Bukoba na Arusha mjini endapo TCAA wataturuhusu kwakuwa tutakuwa na ndege ndogo ambazo zina uwezo wa kutua katika viwanja hivyo,” amesema Masha.
Juzi, TCAA ilitangaza kuwa Fastjet imepoteza sifa ya kufanya biashara nchini na ndege yao moja imezuiwa kuruka kutokana na matatizo iliyonayo na kukosekana kwa meneja mwajibikaji wa shirika. Ilitoa notisi ya siku 28 ikikusudia kuifuta leseni ya shirika hilo.
Comments