Tsunami Indonesia:Watu zaidi ya 40 wafariki dunia na 600 kujeruhiwa
Watu zaidi ya 40 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 600 kujeruhiwa kufuatia mawimbi ya tsunami yenye ukubwa wa mita 20 katika Mlango Bahari wa Sunda, ambayo yameharibu pia majumba kadhaa zikiwemo hoteli za kitalii. Eneo lililoathirika vibaya kwa tsunami hii ni mkoa wa Pandeglang katika jimbo la Banten kwenye kisiwa cha Java, ambacho kina hifadhi ya taifa ya Ujung Kulon na fukwe maarufu, kwa mujibu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Majanga. Katika waliopoteza maisha, 33 wanatokea mkoa huo. Katika mji wa Bandar Lampung kusini mwa kisiwa cha Sumatra, mamia ya wakaazi walihifadhiwa kwenye jengo la ofisi moja ya serikali. Mkaazi mmoja wa wilaya ya Pandeglang aliyejitambulisha kwa jina la Alif alisema wimbi la tsunami kwenye eneo lao lilifikia ukubwa wa mita tatu. Alikiambia kituo cha televisheni cha MetroTV kwamba watu wengi walikuwa bado wanawatafuta jamaa zao waliopotea. "Nililazimika kukimbia wakati wimbi kubwa lilipokiuka ufukwe na kufika umbali wa mita tak...