Posts

Showing posts from December 24, 2018

JITIBU JIPU KWA DAW HII

Image
Bilinganya ni kiungo ambacho hutumika kuongeza / kuleta ladha katika mboga. Pamoja kuwa ni kiuongo ambacho hutumika kuongeza ladha katika mboga pia Ikumbukwe ya kwamba bilinganya ni tunda ambalo ni dawa, ambapo hutumia kutibu magonjwa yafuatayo; Vidonda vya tumbo. Linasaidia sana kwa watu wenye matatizo ya kukosa usingizi wanashauri kula kwa wingi. Pia kwa wale wenye matatizo ya  homa, Ikumbukwe bilinganya husaidia mtu kuwa na afya nzuri ya mwili pindi atakapolitumia. Kwa wale wenye matatizo ya jipu kumbuka ya kwamba bilinginya ni dawa tosha juu ya tatizo hilo, unachotakiwa kufanya ni kwamba lipondeponde kisha uweke katika jibu. Pia kama utaamua kutengeneza jusi yake, inaaminika ya kwamba tunda hili lina uwezo madhubuti wa kuondoa sumu zote zilizopo mwilini. Endelea kutembelea Muungwana Blog kila wakati ili kupata masomo mengine mengi kama haya kila siku. Asante

HABARI ZA LEO 25/12/2018

Image

Chadema kutembeza bakuli kesi ya mbowe

Image
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeanza kuchangishana fedha kuongeza nguvu ya wanasheria katika kesi zinazowakabili wanachama na viongozi wake wakiwamo Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko. Mbowe na Matiko ambao wanakabiliwa na kesi ya uchochezi inayowakabili pamoja na viongozi wengine saba wa chama hicho, walifutiwa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 24 katika ofisi za Chadema Kanda ya Pwani zilizopo Magomeni Makuti, Mwenyekiti wa kanda hiyo, Frederick Sumaye, amesema wanataka haki itendeke haraka ili viongozi hao watoke gerezani waendelee na shughuli zao. “Kanda ya Pwani kwa kuona kwamba mwenyekiti wa taifa yuko ndani tulihitisha mchango wa kusaidia jambo hilo na juzi tulipata Sh 800,000 za kuanzia. “Iringa wanaendelea na michango hiyo na tutandelea kuongeza nguvu ya mawakili. Tunaguswa san

TAARIFA KWA UMMA

Image

Duh! :Baada ya muda mrefu Nape ajitokeza

Image
Jumapili , 23rd Dec , 2018 Na Mwandishi wetu Mbunge wa Mtama na Waziri wa zamani wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ameshindwa kuficha hisia zake juu ya ushindi walioupata timu ya Simba dhidi ya klabu ya Nkana ya Zambia. Nape Nnauye Nkana ambayo ilichuana na Simba leo Jijini Dar es salaam kwenye Uwanja wa Taifa ilishuhudia Simba ikifanikiwa kutinga hatua ya makundi ya michuano klabu bingwa Afrika kwa ushindi wa mabao 3-1. Kupitia ukurasa wake Twitter Nape Nnauye ameandika ameshindwa kujiuzuia moja ya goli lilifungwa na mshambuliaji Clatous Chama na kusema bao hilo ni la aina yake. "Nimejificha vya kutosha, lakini kwa goli hili, Simba hii kiboko This is Simba" aliandika Nape. Watu wengine mashuhuri wakiwemo mastaa wa filamu na muziki wameelezea furaha zao juu ya ushindi wa Simba kama inavyoonekana hapo chini.