Waziri Mkuu Majaliwa ampongeza, Mufti amtaka amalize migogoro yote




Bethsheba Wambura, Dar es Salaam
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kwa kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania, Sheikh Aboubakary Zuberi migogoro ya misikiti imepungua.
Licha ya kupungua huko Waziri Majaliwa amemtaka Sheikh huyo aongeze bidii, ubunifu na kasi kubwa ili afanikishekumaliza migogoro yote inayokabili misikiti nchini.
Akizungumzia umuhimu wa dini Waziri Majaliwa amesema uwepo wa dini mbalimbali nchini ni muhimu  kwa kuwa umesaidia kuunga mkono jitihada mbalimbali za serikali katika kuhakikisha nchi inasonga mbele.
Waziri Mkuu amesema hayo leo Desemba 17, jijii Dar es Salaam katika maadhimisho ya miaka 50 tangu kuaanzishwa kwa Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata).
Amesema kila dini kwa imani zao wanasaidia kutekeleza mambo ambayo kikawaida yangetakiwa kufanywa na serikali.
Akizungumzia sekta ya Afya amesema vituo vya kutoa huduma za afya nchini vimejengwa na taasisi za dini.
“Katika elimu taasisi za dini zikiwamo za waislamu zimejenga vyuo na shule ambazo zinafundisha kuanzia elimu yachekechea. Zimejenga watu wengi wamekuwa na maadili mema ya kujua umuhimu wa uzalendo na mshikamano tangu walipokuwa wadogo,” Amesema na kuongeza.
“Hata utulivu uliopo nchini ni kutokana na dini kuhamasisha amani nchini  kupitia kamati za amani zilizoundwa katika maeneo yote nchini, kupitia makongamano na mikutano yahadhara ya kidini ndio maana hadi leo nchi yetu ina amani kubwa,“ ameeleza Majaliwa.

Comments

Popular posts from this blog

KESI YA ZITTO MUSWADA WA SHERIA YA VYAMA VYA SIASA YAHAMISHWA

Waziri asimamisha likizo za Marubani ATCL