Maalim seif asema: Nitaheshimu maamuzi ya mahakama

Chama cha wananchi cuf kimesema kitaheshimu maamuzi yatakayo tolewa na mahakama kuu kuhusu khatma ya kesi zinazoikabili chama hicho ambazo zitatolewa uwamuzi wake mapema mwakani.

Kesi hizo zinazoikabili chama hicho ni kesi inayohusu msajili wa vyama vya siasa na uruzuku ambayo kesi hiyo  itatolewa maamuzi yeke Januari 15 mwakani na kesi kuhusu kuwepo kwa bodi mbili ya wadhamini ndani ya chama hicho ambayo itatolewa uwamuzi wake February 18 mwakani.

Kauli hiyo imetolewa Juzi na katibu mkuu wa chama hicho Maalim Seif Sharif hamadi wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kikao cha siku buli 16 hadi 28 decembar kilichiojadilihali ya kisiasa nchini,

Maalim Seif alisema chama chake kina uamini muhimili wa mahakama  hivyo maaamuzi yoyote yataayo tolewa wao wamejidhatiti kuweza kuyapokea bila ya kipingamizi cha  aina yoyote.

“maamuzi yoyote yatakayo tolewa sisi na mahakama sisi tumedhitatiti kuweza kuayapokea bila ya kipingamizi ya aina yoyote” alisema Maalim Seif Sharif hamadi.

Aidha Maalim Seif alieleza kuwa Upande  wa chama cha Wananchi wanawake wao wanasubiri tarehe husika iliyopangwa ya kwenda mahakamani kwa maamuzi juu ya kesi zinazowahusu.

Kwa upande alisema vyama vya sita vya siasa vinatangaza kuwa mwaka 2019 kuwa ni mwaka wa kudai Democrasia ambapo watapambana kuzidai haki zao kwa kile wanachoamini kuwa zimepotea kwa muda mrefu haki zao.

kikao hicho kiliwakutanisha wenyevita wa vyama sita vya upinzani ambapo kilifanyika katika hotel verde mjini magharib unguja.

Comments

Popular posts from this blog

KESI YA ZITTO MUSWADA WA SHERIA YA VYAMA VYA SIASA YAHAMISHWA

Waziri asimamisha likizo za Marubani ATCL