HapoKale: Wachaga na kisa cha kurudi nyumbani kila mwisho wa mwaka
Wachaga na kisa cha kurudi nyumbani kila mwisho wa mwaka Wachaga ni kabila lenye asili ya Kibantu na mchanganyiko wa asili ya Kikushi wanaoishi kaskazini mwa Tanzania, Kilimanjaro mkoani Kilimanjaro. Kabila la Wachaga linatajwa kuwa la tatu kwa ukubwa nchini Tanzania, ambapo takwimu za mwaka 2003 zinaonyesha kuwa idadi ya Wachaga ni watu 2,000,000. Shughuli kubwa ya Wachaga ni biashara, kilimo na kazi za ofisini. “Mangi” ni jina waliloitwa watawala wa Kichaga. Hawa walimiliki mashamba, Ng’ombe na waliheshimiwa kama viongozi wa kikabila. Mangi walikuwa na nguvu za kisiasa na utajiri. Baadhi ya Mangi mashuhuri katika historia ni Mangi Rindi aliyeingia mikataba na wakoloni (Wajerumani), Mangi Sina wa Kibosho – anajulikana kwa uhodari wake wa vita katika kupigana na Wamachame na kupora ng’ombe na mazao yao, ...
Comments