Serikali, Airtel zaungana tena
Anna Potinus – Dar es salaam Serikali ya Tanzania na kampuni ya Bharti Airtel zimetia saini mkataba wa umiliki wa hisa na makubaliano hayo yamefikiwa baada ya mazungumzo ya miezi nane baina ya pande hizo mbili. Hafla ya utiaji saini imefanyika leo Januari 15, Ikulu jijini Dar es salaam na Rais Dk. John Magufuli ameshuhudia zoezi hilo ambapo Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi ametia saini kwa niaba ya Serikali na Mwenyekiti wa Kampuni ya Bart Airtel Sunil Mittal aemtia saini kwa niaba ya kampuni yake. Akizungumza baada ya kushuhudia utiaji saini makubaliano hayo Rais Magufuli amesema kwa miaka nane Tanzania ilikua haipati gawio kutoka Bhart Airtel ilihali walikuwa na mkataba nao lakini sasa hali hiyo inaenda kubadilika kutokana na makubaliano waliyoingia. “Miaka yote nane tulikuwa hatupati gawio kutoka Bhart Airtel na ukishaona muda wote huo hatujapata ujue ni biashara mfilisi na ndio maana nilipoingia madarakani tukaliona hili tukasema tuzungumze,” ...