Magufuli atoboa siri barabara za lami


Rais John Magufuli, ametoa siri ya barabara za lami nchini kuwa ni waraka aliouwasilisha kwa Rais Benjamin Mkapa, mwaka 2001.
Amesema waraka huo wa barabara wenye mapendekezo ulipitishwa na Rais Mkapa huku Baraza la Mawaziri likiukataa.
Rais Magufuli mesema hayo leo Jumatano Desemba19, katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi la upanuzi wa Barabara ya Kimara-Kibaha ya Km 19. 2 yenye njia nane.
“Mwaka 2001 kupitia Waraka wa Barabara uliowasilishwa na Waziri wa Ujenzi wakati huo tukapeleka mapendekezo kwenye Barazala Mawaziri, mapendekezo haya sikuyapitisha kwa Katibu Mkuu.
“Wengi hamjui na ujanja niliofanya nilikwenda kumueleza Mkapa, akaniuliza watakubali mawaziri wenzako, akasema wewe ulete usiupeleke kwa makatibu, baadaye ikapelekwa kwenye Baraza la Mawaziri, wote wakaupinga,”amesema.
Amesema waraka huo ulikuwa unasema itengwe Sh bilioni1.14 kwa ajili ya barabara akapewa amri Waziri wa Fedha wakati huo Basil Mramba akaanza kutenga fedha na barabara ya kwanza ilikuwa ya Monduli ilijengwa kwa fedha za ndani.
“Ndipo ikajengwa Barabara ya Nangurukulu hadi Mioyo na ikafungua Barabara ya kutoka Dodoma kwenda Nzega ikawa lami, kutokana na programu hiyo sasa kila mahali ni lami, tumetoka mbali…” amesema Rais Magufuli.
“Nataka kuwaeleza Watanzania tumetoka mbali kutenga bilioni 1.14 ndiyo kumezaa barabara zote hizi na mimi naomba tumpongeze Mzee Mkapa kwa sababu angekataa tusingekuwa hapa,” amesema.

Comments

Popular posts from this blog

KESI YA ZITTO MUSWADA WA SHERIA YA VYAMA VYA SIASA YAHAMISHWA

Waziri asimamisha likizo za Marubani ATCL