Mourinho aacha deni hili Manchester United


Aliyekuwa Kocha wa Manchester United Jose Mourinho hatakuwa na shida ya kuuza nyumba kwa kuwa muda wote aliishi hotelini kama vile machale yalimcheza.

Mourinho ameishi katika jiji la Manchester kwa muda wa siku 895, alikuwa akiishi katika hotel ya Lowry iliyopo jijini humo.

Kwa siku hizo alizoishi hotelini hapo, Mourinho ameacha deni la pauni 537,000 (zaidi ya Sh bilioni 1.5), ambazo zitalipwa na Manchester United.

Aliwasili katika hotel hiyo Julai 6, 2016 kabla ya kufukuzwa na kuondoka katika hotel hiyo Desemba 2018.

Mkewe amekuwa akiishi jijini London na mwanaye wa kike, Matilde amehitimu chuo kikuu cha London na mtoto wake wa kiume, Jose Mourinho Jr alikuwa akiichezea timu ya vijana ya Fulham hadi Aprili 2017.

Comments

Popular posts from this blog

Wanakijiji watishia kumburuza kortini DC

TMA yatoa tahadhari mafuriko yaja