Posts

Showing posts from January 2, 2019

Zuma azua mvutano

Image
4 hours ago Comments Off on Zuma azua mvutano baada ya kupewa msaada wa kurekodi albam yake Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amezua sintofahamu baada ya kupewa msaada na Serikali ya Manispaa kurekodi albam yake ya muziki. Halmashauri ya Manispaa ya Wilaya ya eThekwini kupitia kitengo cha Utamaduni na Urithi imetoa ofa ya kugharamia albam hiyo inayotarajiwa kurekodiwa mwezi Aprili. Albam hiyo inatarajiwa kuwa na nyimbo ambazo zinazungumzia harakati za ukombozi, mapambano kwenye ulingo wa siasa pamoja na maswahibu yaliyowakuta. Chama cha upinzani cha Democratic Alliance kimeeleza kuwa kitamuandikia barua Meneja wa eThekwini kumzuia kutumia fedha za umma kwa ajili ya kufadhili kazi za muziki za Zuma. Diwani wa chama cha Democratic Alliance, Nicole Graham ameeleza kuwa kitengo hicho kilipaswa kutumia fedha hizo kufadhili muziki wa vijana wana...

Bashir Ngangari agoma kuachia Urais

Image
3 hours ago Comments Off on Bashir Ngangari agoma kuachia Urais Rais wa Sudan, Omar al-Bashir amekataa wito wa kujiuzulu nafasi ya urais kufuatia maandamano yaliyozuka kumpinga, pamoja na vyama vya upinzani kujiondoa katika makubaliano ya utawala wa mseto. Chama tawala cha National Congress Party (NCP) kimeeleza kuwa Rais al-Bashir hawezi kujiuzulu. Chama hicho kimesema hatua iliyochukuliwa na vyama vilivyokuwa vinaunda mseto wa utawala ni kinyume cha makubaliano ya majadiliano ya ushirikiano yaliyofikiwa mwaka 2016. Mwishoni mwa juma lililopita, vyama kadhaa vilitangaza kujiondoa kwenye mseto wa utawala na kujiunga na vyama vingine vya upinzani vinavyoratibu maandamano ya kupinga utawala wa al-Bashir nchini humo. Msemaji wa NCP, Ibrahim al-Siddiq ametaja hatua hiyo ya vyama vilivyokuwa kwenye ushirika wa madaraka kama, “kujiondoa kwenye muafaka wa kit...

Somalia na timuatimua

Serikali ya Somalia imemfukuza nchini humo Balozi wa Umoja wa Mataifa, Nickolas Haysom kwa madai kuwa ameingilia mambo ya ndani ya nchi hiyo. Taarifa ya kumfukuza Haysom imemtaka kuondoka mara moja na kwamba hatakiwi tena kurejea ndani ya nchi hiyo akidaiwa kuhoji masuala ambayo ni ya ndani ya nchi yanayoleta sintofahamu. Haymon aliandika barua yenye maswali kadhaa kwa Serikali, akiitaka kutoa maelezo kuhusu kuuawa kwa watu waliokuwa wanaandamana kupinga kukamatwa kwa kiongozi wa zamani wa Al Shabaab, Sheikh Muktari Roobow mjini Baidoa, Desemba 13 mwaka jana. Balozi huyo alitaka kufahamu kuhusu hatua na nguvu iliyotumika na kusababisha kuuawa kwa watu 15 katika mvutano wa kumkamata kiongozi huyo. Barua hiyo iliyoelekezwa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi hiyo, ilitaka kufahamu kuhusu ushiriki wa wanajeshi ambao wanaungwa mkono na Umoja wa Mataifa katika kukamatwa kwa Roobow. Alifafanua kuwa, kwa mujibu wa taratibu na mikataba ya kimataifa, usaidizi wa majeshi ya Umoja wa Ma...

Siasa safi si kuhama chama

Image
LEONARD MANG’OHA TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) hivi karibuni imemtangaza mgombea ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Mtolea, kuwa Mbunge wa Temeke, nafasi ambayo alikuwa anaishikilia kipindi akiwa mwanachama wa Chama cha Wananchi -CUF . Tofauti ya ubunge wa sasa na ule aliouvua ni kwamba mara hii amepita bila kupingwa baada ya washindani wake kuondolewa katika kinyang’anyiro hicho kwa kukosa sifa. Kutokana na washindani hao kukosa sifa NEC, imelazimika kumtangaza kuwa mshindi bila hata kwenda katika masanduku ya kupigia kura, na kutoa haki kwa wananchi kumchagua kiongozi wao wanayemtaka. Kitendo cha Mtolea kutangazwa na tume hiyo kushika nafasi hiyo bila kupigiwa kura si cha kushangiliwa si tu na wafuasi wa chama chake kipya bali pia yeye mwenyewe, kitendo hicho kinaondoa dhana ya demokrasia na haki ya kuchagua na kuchaguliwa. Mtolea hapaswi kuufurahia ubunge huo ambao hajautolea jasho. Heshima aliyokuwa nayo awali siamini kama itaend...

Mvua ya dakika 45 yazua makubwa

Image
Na IBRAHIM YASSIN-MBOZI MVUA kubwa iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha kwa dakika 40 wilayani hapa, imesababisha nyumba 56 kuezuliwa huku watu tisa wakijeruhiwa. Tukio hilo lilitokea katika Kijiji cha Utambalila, Kata ya Nambizo wilayani Mbozi mkoani Songwe. Mbali na maafa hayo, pia mali kadhaa ziliharibiwa. Akizungumza jana na gazeti hili, mmoja wa waathirika hao, Simwinga Mwashambwa alisema alfajiri ya jana walisikia mirindimo na vishindo vikubwa na walipotoka nje walikuta mabati yanapeperushwa na upepo, kuta zikianguka, mazao yaliyotunzwa vyote vikizama majini. Alisema baadaye walitoa taarifa kwa uongozi wa kijiji na kushauriana wakimbilie katika shule ya msingi iliyopo kijijini hapo. “Kwa sasa tunahitaji msaada zaidi ili tuweze kujenga nyumba na kurudi kwenye makazi yetu maana hata mazao tuliyotunza kwa chakula na mbegu yameharibiwa na maji ya mvua, tunahitaji msaada wa haraka,’ ’alisema Mwashambwa huku akitokwa na machozi. Ofisa Mtend...

Lukuvi asema haya

Image
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya  Makazi, William Lukuvi, amesema chanzo cha baadhi ya nchi wahisani kugomea kutoa misaada kwa Tanzania kunatokana na msimamo wa Rais Dk. John Magufuli kuhusu kulinda rasilimali za nchi. Kwa mujibu wa Lukuvi msimamo huo haujazifurahisha nchi hizo na kuamua kuweka masharti magumu katika misaada yao kwa Tanzania. Waziri Lukuvi, alitoa kauli hiyo usiku wa kuamkia jana, wakati wa mkesha wa kukaribisha mwaka mpya  wa 2019, uliofanyika Kariakoo, Dar es Salaam ambapo alimwakilisha Rais Magufuli. Waziri Lukuvi, alisema pamoja na hali hiyo, bado Serikali imeendelea kuwa imara na kuhakikisha inakusanya kodi za ndani ili kuweza kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo ikiwamo ya umeme wa maji wa Rufiji (Stiegler’s Gorge).   “Leo (jana) tupo kwenye mkesha hapa, hakika nawaomba endeleeni kumwombea kwa dhati Rais Magufuli ili Mungu azidi kumpa nguvu na baraka za kuliongoza Taifa letu. “Mnakumbuka hivi karibuni Ta...