Songea kukopesha Wanawake na Vijana kukwama
on Songea yakwama kukopesha Wanawake na Vijan Manispaa ya songea mkoani Ruvuma, imeshindwa kuendelea kukopesha vikundi vya wanawake na vijana kupitia mapatoyake ya ndani, baada ya vikundi hivyo kushindwa kurejesha fedha za mikopo kwa wakati na vinadaiwa zaidi ya sh. milioni 59. Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Tina Sekambo ametoa taarifa katika kikao cha kamati ya ushauri na maendeleo ya mkoa wa Ruvuma (RCC), kuwa vikundi vilivyoshindwa kurejesha mikopo vingi vilikopeshwa katika kipindi cha mwaka 2017/18, na hadi kufika mwezi novemba 2018, na nikikundi kimoja pekee ambacho kimeweza kupunguza deni lake. Katika kipindi hicho cha miaka miwili manispaa hiyo imeweza kuwakopesha wanawake na vijana fedha kupitia makusanyo yeke ya ndani asilimia 10 kila mwezi, ambapo sh. milioni 31.10 zimekopeshwa kwa vikundi vya wanawake, na vijana sh. milioni 28.1. kwa lengo la kupambana na umasikini kwa njia ya ujasiriamali kwa kufanya kazi za mikono, ikiwemo kilimo na biashara ndogo ndogo ili waweze k...