Mkuu wa Utawala wa Polisi Mkoa wa Mwanza, ACP Advera Bulimba M WANZA: Tukio la Jeshi la Polisi jijini Mwanza kukamata kilo 323.6 za dhahabu na maburungutu ya fedha taslim kiasi cha shilingi milioni mia tatu na milioni tano (305,000,000), Jumamosi iliyopita, limeibua sintofahamu na utata mkubwa uliotawaliwa na maswali, Uwazi limedokezwa. Taarifa za awali zilidai kuwa dhahabu na mamilioni hayo ya shilingi yalikuwa yakisafirishwa kuelekea mkoani Geita. Katika tukio hilo ambalo watuhumiwa watatu wanashikiliwa na jeshi hilo, dhahabu ilikamatwa ndani ya gari katika Kivuko cha Kigongo huku mamilioni hayo yakinaswa ndani ya gari kwenye Kivuko cha Kamanga jijini Mwanza. Kufuatia matukio hayo mawili, kuliibuka maswali mengi yenye utata na kwamba itakuwa ni miongoni mwa kesi zitakazovuta hisia za wengi kutokana na kiasi hicho kikubwa cha dhahabu na pesa zilizonaswa. “Mimi ninachojua ni kwamba mtu ukitaka kusafirisha kiasi kikubwa cha fedha lazima uombe ulinzi wa ...