WAZIRI Kivuli, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Esther Bulaya amemtaka Waziri Jenista Mhagama ajali misingi ya uwajibikaji kwa kujiuzulu wadhifa wake kutokana na kushindwa kusimamia masilahi ya wafanyakazi. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Bulaya ambaye ni Mbunge wa Bunda (Chadema), alisema hatua ya Rais Dk. John Magufuli kutengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka na kuwaacha wengine wanaotakiwa kuwajibika imeibua utata, kwa kuwa mkurugenzi huyo ni mtendaji tu. Alisema sheria ya mafao ya mwaka 2018 imempa Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu mamlaka ya moja kwa moja ya kutunga na kusimamia kanuni za ukokotoaji wa mafao, hivyo Jenista anatakiwa kuwajibika au laa awajibishwe kwa kutojali maoni ya wadau wakati wa utafutaji na upitishaji wa kikokotoo ambacho Rais Magufuli alikitengua. “Kutengua uteuzi wa Mkurugenzi wa SSRA na...