Posts

Showing posts from December 14, 2018

Serikali ya wanyonge mnatusikia wanyonge?

Image
na EMMANUEL MWANSASU WANYONGE wanyonge wanyonge, neno wanyonge linasikika sana miaka ya karibuni haswa tangu awamu hiii ingie madarakani na Serikali yetu imekuwa ikijinasibu mara nyingi kuwa hii ni Serikali ya wanyonge lakini bado nina mashaka kama kweli Serikali hii ya wanyonge inatusikiliza wanyonge. Ukitaja wanyonge kwenye nchi hii basi unataja namba kubwa ya watu ambayo inaweza kuchukua zaidi yaasilimia sitini na kama hukubaliani na hili hebu fanya utafiti mdogo kwenyesehemu zinazotoa huduma za kijamii, ukiangalia kwa sehemu kubwa utaona wananchi wengi wa hali ya chini hukimbilia kwenye vituo vya umma leo hii ukienda Kairuki Hospitali huduma inayotolewa pale si sawa na huduma inayotolewa Mwananyamala Hospitali,namba ya watu utakayoikuta katika hospitali hizo mbili ni tofauti kabisa hapo hujatembelea shule za Kayumba almaarufu shule za Kata ulinganishe na shule kamaAl Muntazir na nyinginezo, hivyo mara nyingi ninapokuwa nasikia serikali ya wanyonge itatupigania wanyon