Posts

Showing posts from December 21, 2018

Magufuli ataka jina libadilishwe

Image
Alhamisi , 20th Dec , 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli ameitaka mamlaka inayosimamia ujenzi wa wa Daraja la Selander kubadilisha jina hilo na kutoliita kwa jina la mtu, badala yake wanapaswa kubuni jina ambalo litaitangaza Tanzania. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli Akizungumza katika uzinduzi wa uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa daraja hilo, Dk. Magufuli amesema kwamba jina la daraja hilo linapaswa kutangaza nchi haswa ikizingatiwa kuwa daraja hilo lipo maeneo ya ubalozi wa mataifa mbalimbali hivyo itakuwa rahisi kwao kusafiri kwa haraka. " Hili jina la daraja 'New Selander Bridge', nafikiri mngelibadilisha na kuliita jina lingine ambalo litaitangaza Tanzania vizuri kimataifa. Hata mngeliita Tanzanite, kwani ni madini pekee yanayopatikana Tanzania ila msiite jina la mtu ". Pamoja na hayo Rais Magufuli ameongeza kwamba " Mwalimu Ny...

TIZAMA HII 2018

Image
This $99 Drone Is The Most Incredible Invention of 2018 Summary: This brilliant new drone is taking the world by storm . It lets you take stunning photos and videos from above, so you can impress your friends on your next vacation. You can take it with you anywhere thanks to its compact size. Its so easy to use that you can have it ready to go in under 30 seconds. The best part? DroneX Pro focuses on product development instead of branding. This means they're able to offer a world-class quality drone at an incredibly low price. "The reason brand name drones are so expensive isn't because of their technology. It's because of their brand name." -Engineer for DroneX Pro Over the last 12 months we've tested most of the drone models on the market. Typically models under $100 are very difficult to control even in light wind. Their camera also struggles to deliver high-quality photos and videos. However in the last few months, a cheap drone m...

Rais azitafuta fedha zilizojenga nyumba hewa

Image
Ijumaa , 21st Dec , 2018 Na Mwandishi wetu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Maguful, amebainisha sababu za kufanya mabadiliko kwenye Jeshi la Magereza kuwa ni kutokana kutoa fedha ambazo aliagiza kujengwa kwa nyumba za maaskari lakini mpaka sasa hazijajengwa. Rais Magufuli Rais Magufuli ametoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam wakati akizungumza kwenye hafla ya utoaji vyeo kwa wahitimu wa maofisa na Ukaguzi, ambapo ameshangazwa kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya askari magereza lakini hakuna iliyojengwa. " Kule Magereza nilitoa pesa kwa ajili ya kujenga nyumba za askari magereza pale Ukonga, zile nyumba mpaka leo hazipo na hela zimeisha, ndiyo maana nilifanya mabadiliko haraka haraka pale ". " Niwaeleze ukweli huwa ninauvumilivu lakini uvumilivu wa kwenye fedha huwa unanishinda, unatoa nyumba kwa ajili ya maaskari lakini hakuna kinachojengwa, nimemuagiza Kamishna Magereza azifuatilie h...

Wanne mbaroni kwa kubaka 'mtungo'

Image
Ijumaa , 21st Dec , 2018 Na Mwandishi wetu Wanawake wanne (majina yamehifadhiwa) wakazi wa kijiji cha Buganzu kata ya Lunzewe Mashariki, Wilayani Bukombe Mkoani Geita wamebakwa na wanaume zaidi ya mmoja baada ya kuvamiwa na watu hao wakiwa majumbani mwao. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwalubambo. Tukio la kubakwa wanawake hao limetokea Desemba 11 majira ya saa nane usiku katika kijiji hicho, walipovamiwa na wanaume wanne wakiwa wamelala kisha kubakwa na kila mmoja na kupelekea kuwasababishia maumivu makali. Akizungumza Mkoani Geita Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwalubambo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba watuhumiwa waliofanya unyama huo wamekwishakamatwa ambapo amewataja kuwa ni pamoja na George Deogratius(42) maarufu (Tolu) mkazi wa Ibamba, Josephat Emmanuel(25) mk...

Sirro-Tumejipanga uchaguzi wa 2020"-

Ijumaa , 21st Dec , 2018 Na Fatuma Muna Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon N. Sirro amesema Jeshi hilo limejipanga vya kutosha kusimamia usalama katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika na ule wa 2020.                                                         Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon N. Sirro. Kamanda Sirro ameyasema hayo leo Disemba 21, 2018 katika mahafali ya kuhitimisha mafunzo ya maofisa na wakaguzi wasaidizi wa polisi, ambapo ameweka wazi kwamba hawatatoa nafasi kwa mtu yeyote kuhatarisha amani ya nchi ya Tanzania. “ Tumejipanga vizuri kuhakikisha uchaguzi unakwenda vizuri. Siku zote huwa nasema kama unaamua kuchukua silaha ya AK 47 ambayo haipatikani duka ...

Ndege tatu chuo cha NIT

Image
Na NORA DAMIAN-DAR ES SALAAM CHUO cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kinatarajia kununua ndege tano za mafunzo kukabili upungufu wa rasilimali watu katika sekta ya anga nchini, hasa marubani. Ndege hizo zitanunuliwa mwakani kwa ushirikiano wa Serikali na mkopo wa Dola za Marekani 21,250,000 ambazo ni takribani Sh bilioni 48.8 ambao chuo hicho umepata kutoka Benki ya Dunia (WB). Akizungumza jana wakati wa mahafali ya 34, Mkuu wa chuo hicho, Profesa Zacharia Mganilwa, alisema mradi huo utakaoanza Februari mwakani unalenga kukiwezesha chuo hicho kuwa kituo cha umahiri cha mafunzo ya marubani, wahandisi wa matengenezo ya ndege na wahudumu wa ndani ya ndege. “Sekta ya anga kwa sasa inakua kwa kasi kwa wastani wa asilimia 12 kwa mwaka na rasilimali watu katika sekta hii ina changamoto nyingi na kubwa. “Tunaendelea kutoa mafunzo ya uhandisi wa matengenezo ya ndege, mafunzo ya wahudumu wa ndani ya ndege na tupo katika hatua za mwisho za maandalizi ya mafunzo ya urubani...

Makonda anusurika mtego wa JPM

Image
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameukwepa mtego wa Rais Dk. John Magufuli kuhusu hatima ya ufukwe wa Coco. Hatua hiyo inatokana na uamuzi wake wa kuanza kueleza mikakati itakayofanyika, ikiwamo kuundeleza ufukwe huo sambamba na kujenga mabanda kwa wafanyabiashara na vyoo vya kisasa. Kutokana na maelezo hayo ya utangulizi, Rais Magufuli alisema amemkwepa kwa kumuwahi kwani ilikuwa kuna uamuzi mgumu dhidi yake. Alisema ufukwe huo wa Coco unatia aibu kwa sababu hakuna hata choo hali ya kuwa mapato yanakusanywa kila siku. Mkuu huyo wa nchi alitoa kauli hiyo jana Dar es Salaam, wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la kisasa la Selander ambalo linapita baharini. “Nimefurahi maneno ya RC (Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda) kuwa wataboresha pale Coco Beach kuliko kukaa vile kwa sababu panatia aibu kwa jiji kama la Dar es Salaam. “Eneo lile halina hata choo, ni lazima tuzizungumze aibu, lakini wanakusanya mapato kila ...

Mvua, upepo mkali waleta maafa

Image
KAYA 50 za vijiji vinne vilivyopo Kata ya Ivuna, Tarafa ya Bonde la Kamsamba, Wilaya ya Momba mkoani Songwe wameingia katika hali ya sintofahamu baada ya nyumba zao kuezuliwa na na upepo mkali ulioambatana na mvua kubwa. Maafa hayo yamesababisha uharibifu wa mazao ya chakula, hivyo kuna hatari familia hizo kukosa chakula na mahali pa kuishi. Mmoja wa waathirika hao, Difris Sikumbulu alisema mvua iliyonyesha siku mbili mfululizo imesababisha nyumba kuezuliwa na chakula kusombwa na maji. Alisema kutokana na hali hiyo, hawana uhakika wa chakula na hata uwezo wa fedha kuzijenga upya nyumba zao au kuzikarabati bado ni mtihani, hivyo wanaiomba Serikali na wadau mbalimbali kuwapatia msaada unaowezekana. Ofisa Tarafa ya Kamsamba, Zakayo Mwasomola alisema maafa hayo yalitokana na mvua kunyesha siku mbili mfululizo ikiyoambatana na upepo.  Alivitaja vijiji vilivyokumbwa na maafa hayo kuwa ni Mkonko, Samang’ombe, Kasamba na Lwati. Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa ...

Wawili kizimbani waponzwa na WhatsApp

Image
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ardhi, Anna Mwaisumo (23) na mpenzi wake Samson Kisuguta (28), wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka manne ikiwemo ya kulawiti na kusambaza picha za ngono kwenye mtandao wa kijamii wa WhatsApp. Mwaisomo ambaye makazi yake ni kwenye Hosteli za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) huku Kisuguta ni mkazi wa Msasani na mfanyabiashara walifikishwa mahakamani hapo leo Ijumaa mbele ya Hakimu Mkazi, Salim Ally. Wakili wa Serikali, Mwanaamina Kombakono akisaidiana na Janeth Magohe alidai kuwa washitakiwa hao walitenda makosa hayo kati ya mwaka 2017 na mwaka huu maeneo ya Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam. Magohe alidai katika mashitaka ya kwanza kuwa, washitakiwa wote kwa pamoja katika tarehe na mahali kusikofahamika mwaka jana, ndani ya jiji hilo, walikula njama kutenda kosa la kulawiti, kuchapisha picha za ngono na kulazimisha kupata fedha ili kutochapisha picha hizo. Alidai katika mashtaka y...

CCM yatoa neno uhakiki wa taarifa za wakulima wa korosho

Image
Na.Ahmad Mmow,Nachingwea. Chama Cha Mapinduzi(CCM) wilaya ya Nachingwea,mkoa wa Lindi kimeshauri timu ya uhakiki wa taarifa za wakulima wa korosho katika wilaya hii iwe makini ili kuepuka malalamiko kutoka kwa wananchi. Ushauri huo ulitolewa jana na katibu wa CCM wa wilaya ya Nachingwea,Rafael Mwita wakati wa kikao cha kamati ya ushauri ya wilaya(DCC) kilichofanyika katika mamlaka ya mji mdogo wa Nachingwea. Mwita ambaye katika kikao hicho alikuwa nimiongoni mwa wajumbe waalikwa,alisema japokuwa uundwaji wa timu hiyo ya uhakiki unania njema ya kutekeleza agizo la Rais kuhusu uhakiki wa taarifa za wakulima wa korosho.Hata hivyo timu hiyo inatakiwa kuwa makini ili kuepuka migongano na malalamiko. Alisema wakati zoezi hilo linaendelea,tayari zimeanza kutolewa tafsiri tofauti kutokana na kasi ndogo ya malipo ya wakulima wa zao hilo.Ikielezwa kwamba zoezi hilo nimiongoni mwasababu zinazosababisha ucheweshaji malipo. Aidha Mwita aliishauri timu hiyo kuwa makini k...

Wolper aogopeshwa

Image
 Muigizaji wa filamu nchini Tanzania, Jacquiline Wolper amefunguka juu ya kuweka wazi mahusiano yake kwenye mitandao ya kijamii. Wolper katika mahojiano yake na Dizzim Online, amesema kuwa ukiwa unaposti mtu ambaye uko nae kimapenzi inakuwa rahisi wabaya wako kumuiba hasa mtu akiwa na makalio makubwa. "Unajua kitu kimoja tunshindwa kuelewa wadada ambao tulikuwa tuna expose mapenzi yetu kuna mtu tu ana matamanio yake anachuki na wewe anaona aah huyu Wolper anatupostia bwana ake sasa na mimi na hili kalio langu ngoja nikamchukue yule bwana sijui unanielewa hana mapenzi na bwana ako anakuja tu kukukomesha kwahiyo upostiji wako, " amesema Wolper. "Unafanya wale wa baya wako watafute pa kukuumiza, Wale wanaonyakuliwa hawajui kwamba nimependwa na nimetakiwa kwaajili yako kwasababu wao wana watu wao hawataki kuwa expose."

Pigo kubwa upinzani sherehe za krismas na mwaka mya

Image
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko wamewatakiwa wanachama wao heri ya Sikukuu ya Krismasi na Mwaka mpya huku wakirudishwa rumande. Wawili hao wametoa heri hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mara baada ya kuahirishwa kwa kesi yao ya uchochezi inayowakabili na viongozi wengine saba wa chama hicho. Wakili wa Serikali, Wankyo Simon, amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu. Wilbard Mashauri kuwa kesi imekuja kwa ajili ya kutajwa. Wakili Simon amedai kuwa hawana taarifa ya kinachoendelea Mahakama ya juu hivyo wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa. Hata hivyo, Wakili Faraja Mangula alidai kuwa Wakili wa washitakiwa hao. Peter Kibatala na Sheck Mfinanga wamepata dharura hivyo wanaomba mahakama ipange Januari 4, mwakani. Akijibu hoja hiyo, Wakili Simon amedai wanaiachia Mahakama ipange tarehe itakayoona inafaa. Hakimu Mashauri amesema Januari 4, mwakani atakuwa na kazi nyingine hivyo aliahirisha kesi hiyo hadi Januari ...

Rais JPM aaga msiba wa aliyekuwa makamu mkuu wa chuo kikuu cha dodoma

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli ameaga Mwili wa Marehemu, Profesa Egid Beatus Mubofu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dodoma nyumbani kwakwe Tabata wilaya ya Ilala. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.John Pombe Magufuli akitoa heshima zake za mwisho kwa Marehemu Profesa Egid Beatus Mubofu aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM) mara baada ya kuwasili Tabata Wilaya ya Ilala nyumbani kwa marehemu, aliyefariki dunia Desemba 18,2018 Nchini Afrika Kusini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.John Pombe Magufuli akimpa pole Bi.Joyce Chamhuro (Mke wa Marehemu) pamoja na familiya ya Marehemu Profesa Egid Beatus Mubofu aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM) , mara baada ya kuwasili Tabata Wilaya ya Ilala nyumbani kwa marehemu, aliyefariki dunia Desemba 18,2018 Nchini Afrika Kusini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.John Pombe Magufuli akitia saini ...

Wanaosambaza nyaraka za serikali bila idhini wapigwa marufuku

Image
Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha amesema ni kosa kusambaza nyaraka za serikali katika mitandao ya kijamii bila idhini ya Mamlaka husika, hivyo ameagiza kuchukuliwa hatua za kinidhamu na za kisheria kwa watumishi watakaobainika kusambaza nyaraka hizo. Naibu Waziri Ole Nasha ametoa agizo hilo mkoani Morogoro wakati akifunga semina ya mafunzo ya Huduma kwa Mteja na Utunzaji wa Kumbukumbu kwa baadhi ya Maafisa wa Wizara hiyo na kusisitiza kuwa hakuna mtumishi yeyote wa serikali asiyefahamu kuwa kutoa nyaraka za serikali bila idhini ni kosa la jinai. “Kumekuwa na usambazaji wa nyaraka za serikali katika mitandao ya kijamii bila idhini na kwa bahati mbaya wakati mwingine unakuta nyaraka imewekwa mhuri wa siri lakini bado unaikuta huko, watumishi wa serikali lazima watambue kuwa kuna utaratibu wa kutoa nyaraka za serikali na kuna sheria ambazo zinawabana wale wote wanaotoa taarifa hizo bila kuidhinishwa”alisisitiza Naibu Waziri O...

MAGAZETI YA LEO 22/12/2018

Image

MATOKEO ACSEE 2018 HAYA HAPA

NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA ACSEE 2018 EXAMINATION RESULTS ENQUIRIES CLICK ANY LETTER BELOW TO FILTER CENTRES BY ALPHABET ALL CENTRES A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z P0101 AZANIA CENTRE P0104 BWIRU BOYS CENTRE P0110 ILBORU CENTRE P0112 IYUNGA CENTRE P0116 KANTALAMBA CENTRE P0119 KIBAHA CENTRE P0123 KWIRO CENTRE P0129 MARA CENTRE P0132 MILAMBO CENTRE P0133 MINAKI CENTRE P0134 MOSHI CENTRE P0135 MOSHI TECHNICAL CENTRE P0136 MUSOMA CENTRE P0140 MZUMBE CENTRE P0143 NJOMBE CENTRE P0145 NYAKATO CENTRE P0147 PUGU CENTRE P0150 SAME CENTRE P0151 SENGEREMA CENTRE P0152 SHINYANGA CENTRE P0153 SONGEA BOYS CENTRE P0156 TANGA TECH. CENTRE P01...