Posts

Showing posts from December 27, 2018

Huyu mama aamua kusema!

Image
Mchungaji wa Kanisa la Assemblies Of God maarufu kama ‘Mlima wa moto’ Dk Getrude Rwakatare, amemshukuru Rais Magufuli kwa kumgundua Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam. Mama Rwakatare amesema kuwa kwa mara ya kwanza alimuona Makonda ana bidii ya tofauti na jasiri. "Namshukuru Rais wetu kwa kumgundua Paul Makonda , mimi nakumbuka nilikumgundua akiwa kiongozi wa Wana vyuo pale Moshi alivyonialika kwenye mkutano mkubwa kabisa wa wana vyuo," alisema Mama Rwakatare. "Nilimuona ana bidii ya tofauti na ujasiri wa tofauti, niliona kwamba Mungu amempa wito ndani yake, nilikuiwa nasema Mungu naomba utokee mahali fulani kiwa bahati tukakutana tena kwenye Bunge la Katiba." Mama Rwakatare ameyasema hayo katika hafla ya viongozi wa dini iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda ya kupata chakula cha pamoja.

Kigogo mwendokasi, wenzake waachiwa kwa dhamana

Image
Na MWANDIDHI WETU – DAR ES SALAAM WAFANYAKAZI saba wa Kampuni ya Uda-Rapid Transit (UDART), akiwamo kigogo wa idara ya fedha, wanaodaiwa kuhusika katika mtandao wa uhujumu wa mapato ya mabasi ya mwendokasi kwa kuchapisha tiketi feki kwa abiria wameachiwa kwa dhamana. Hatua hiyo imekuja baada ya kushikiliwa kwa zaidi ya siku 60 na Jeshi la Polisi huku wakiendelea kusubiri uamuzi wa jalada lao ambalo lipo kwa mwanasheria mkuu wa Serikali, likisubiri hatima yao kama kufikishwa mahakama ama laa. Pamoja na kuachiwa, wafanyakazi hao ambao awali walikuwa wanane wametakiwa kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi mara kwa mara huku upelelezi wa kesi yao ukiendelea. Akizungumza na MTANZANIA jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alisema tuhuma zinazowakabili wafanyakazi hao ni za kughushi na kuhujumu mapato ya mradi wa mabasi ya mwendokasi, hivyo upelelezi wake unachukua muda mrefu ili kuhakikisha wanapata mtandao mzima. Alise...

kumbuka mambo haya

Image

Aliyetekwa kwa miaka 30 apatikana

Image
Alhamisi , 27th Dec , 2018 Na Mwandishi wetu Mwanamke mmoja raia wa Argentina ameokolewa na polisi baada ya kushikiliwa mateka kwa zaidi ya miaka 30. Mwanamke aliyeokolewa na polisi baada ya kushikiliwa mateka kwa miaka 30 (wapili kushoto) na mwanae wa miaka tisa wameungana na familia yao. Operesheni ya kumnasua mwanamke huyo ilifanyika kwa ushirikiano wa polisi wa nchi za Argentina na Bolivia. Mahala ambapo alikuwa akishikiliwa mwanamke huyo ambaye sasa ana umri wa miaka 45 lilikuwa halifahamiki toka miaka ya 80. Hata hivyo, mapema mwaka huu, polisi walipata taarifa kuwa alikuwa akishikiliwa katika eneo la Bermejo, kusini mwa Bolivia baada ya uchunguzi, polisi walifanikiwa kuitambua nyumba aliyokuwemo na kufanikiwa kumuokoa akiwa na mtoto wake mwenye umri wa miaka tisa. Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji katika taarifa iliyotolewa na polisi nchini Argentina wanasema mwanamke huyo amefanikiwa kurejeshwa na kuungana na...

Krismasi yawa hatari Kagera

Image
Alhamisi , 27th Dec , 2018 Na Mwandishi wetu Watu wanne wamefariki dunia mkoani Kagera katika kusherehekea sikukuu za Krismasi na siku ya Boxing Day , kufuatia matukio manne yaliyotokea kwa nyakati tofauti mkoani humo. Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Revocatus Malimi, lipo tukio la Desemba 25 katika kijiji cha Kigorogoro wilaya ya Kyerwa, mwanamke alipigwa na mpenzi wake wakati wakisherehekea sikukuu hiyo kwenye moja ya majumba ya starehe, ambapo mwanaume huyo alimtuhumu mpenzi wake kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine. Katika tukio la pili Kamanda huyo amesema kuwa Justus Clemence mwenye umri wa miaka 42 mkazi wa kitongoji cha Itokozi wilayani Biharamulo anayedaiwa kuwa na ugonjwa wa akili, alipoteza maisha baada ya kupigwa na watu waliomtuhumu kuiba kondoo wa mwanakijiji mwenz...

UVCCM wampitisha mgombea Urais CCM 2020

Image
Alhamisi , 27th Dec , 2018 Na Mwandishi wetu Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, kupitia kwa Katibu wa idara ya uhamasishaji na chipukizi Hassan Bomboko, imesema kuelekea uchaguzi wa mwaka 2020 umoja huo utaenda Dodoma kuhakikisha Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wa sasa Rais John Pombe Magufuli, anapewa Umoja wa Viajana wa Chama Cha Mapinduzi UVCCM wakiwa kwenye kikao. nafasi ya kuwania tena Urais. Kwa mujibu wa Bomboko kwenye kikao kitakachofanyka Dodoma Umoja huo hautakuwa na lengo jingine zaidi ya kumpitisha Rais Magufuli kuwania tena nafasi hiyo ya kukiongoza chama hicho kwenye uchaguzi wa awamu ya pili. " Kama msemaji rasmi wa UVCCM, msimamo wa taasisi yetu ni kwamba hatuna na hatutakuwa na mchakato wa kumtafuta mgombea Urais 2020 mwingine zaidi ya Magufuli ambaye ndiyo Mwenyeki...

VIDEO: Walalamikia hali kibiashara kuwa ngumu

Image
Wafanyabiashara wa maduka katika stendi ndogo jijini Arusha wamefunguka na kuelezea hali ya kibiashara katika kipindi hiki cha sikukuu ya krismas na mwaka mpya kwamba ni ngumu kuliko mika iliyopita ilikuwa na afadhali. Akizungumza Katibu wa wafanyabiashara stendi ndogo jijini Arusha  Anjelo Shokia  amesema kuwa kwa hali hiyo itapelekea wengi kufunga biashara na kutafuta vitambulisho ili kurudi hali ya kuwa wamachinga.

VIDEO: Maalim Seif kutua ACT Wazalendo siri yafichuka, CUF waeleza A-Z

Image
 Mkurugenzi wa Ulinzi wa Chama cha Wananchi (CUF), Khalifa Suleiman amefunguka kuhusiana na sakata la Katibu Mkuu wa chama hicho Maalim Seif kuhamia ACT Wazalendo.

VIDEO: Serikali ya JPM yapongezwa kwa kupanua wigo wa ajira

Image
  Baadhi ya wamiliki wa vituo vya mafuta jijini ARUSHA wamesema usimamizi mzuri wa serikali katika biashara hiyo umeweza kuifanya sekta hiyo kuimarika na kutoa fursa kwa Watu kuwekeza katika sekta hiyo jambo linaloweza kuongeza wigo wa ajira kwa vijana.

Messi na Ronaldo waburuzwa na samatta

Image
Messi, Samatta na Ronaldo. Mbwana samatta amechomoza katika orodha ya majina ya vinara wa mabao Cristiano Ronaldo  na Lionel Messi ambapo mpaka wakati wa Krismasi na Mwaka mpya walikua wanaongoza lakini kwa mwaka huu imekua tofauti. Samatta ambaye ni nahodha wa Tanzania amejihakikishia kuwazidi Messi na Ronaldo kwa mabao ya ligi mpaka sasa baada ya jana kufunga bao 1 kwenye ushindi wa mabao 3-1 wa KRC Genk dhidi ya K.A.A. Gent jana. Kupitia bao hilo Samatta alifikisha mabao 15 hivyo kuwazidi Messi na Ronaldo ambao hawajafikisha idadi hiyo ya mabao. Ronaldo ana mabao 12 huku Messi akiwa na 14. Kwa mujibu wa ratiba ya ligi kuu ya Italia, Juventus imebakiza mechi moja kabla ya mwaka 2018 kumalizika ambapo itacheza dhidi ya Sampdoria Desemba 29 hivyo Ronaldo anahitajika kufunga mabao 3 ili kumfikia Samatta. Kwa upande wa Barcelona, wao hawatakuwa na mchezo mpaka mwakani hivyo Messi atabaki na mabao yake 14 ya ligi na kumwacha Samatta akiwa na mabao 15. Si...

Tundu Lissu kurudi Tanzania

Image
Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu. Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu amebainisha kuwa katikati ya mwaka 2019, anaweza kurudi nchini kwa ajili ya kuendelea na shughuli zake za kisiasa baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 Mwanasheria huyo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ametoa kauli hiyo akiwa anaendelea na matibabu nchini Ubelgiji. Lissu amesema "katikati ya mwakani naweza kurudi Tanzania, kuanza mazoezi hakutanizuia kurejea kwani naweza kurudi nyumbani na nikawa nakuja Ubelgiji kwa madaktari." Aidha kuhusiana na kugombea nafasi ya Urais kwenye Uchaguzi Mkuu 2020 Mwanasheria huyo wa CHADEMA amebainisha kuwa yuko tayari kukiwakilisha chama chake kwenye kinyang'anyiro hicho. "Wakikaa katika vikao na kunipa bendera ya kukiwakilisha chama changu, nitakubali kubeba msalaba huo mzito kwa mikono miwili" amesema Lissu.