Posts

Showing posts from December 15, 2018

Mfahamu kigogo na mgunduzi wa simu ya kwanza

Image
Nafahamu fika bila shaka mawasilaiano ya simu yamekusaidia mambo mbalimbali. Pamoja na kukusaidia mambo hayo mbalimbali swali langu kwako je umfahamu mgudunzi wa simu? Kama jibu ni hapana, basi fahamu ya kwamba bwana Alexender Graham Bell huyu ndiye mgunduzi wa simu ya kwanza kabisa. Alexender Graham Bell yeye alizaliwa mnamo mwaka 1847 katika mji wa Edinburgh nchini Uskoti na baadae alihamia nchi za kanada. Baba yake na mgunduzi huyu wa simu alikuwa ni mwalimu wa wanafunzi wenye ulemevu wa kusikia yaani viziwi baadae elexender naye ajilijikuta anakuwa na mgunduzi na mvumbuzi wa vitu mbalimali. Wakati mkewe ndiye aliye mvutia na kumshawishi Alexander Graham Bell aweze kuzama ndani zaidi kiuchunguzi kwa kufanya uchunguzi katika matamshi na usikilizaji baadae alikwenda zaidi kuchunguza ni jinsi gani vifaa vya kusikilizia sauti hufanya kazi hapo ndipo alipo weza kuibuka na simu yakwanza yenye kufanya kazi. Alizawadiwa tuzo iliyo fahamika kama first U.S patent mnamo mwak

zitambue faida za kutumia mchaichai kama tiba na chakula

Image
Zifuatazo ni faida za kutumia mchaichai kiafya. 1. Mchaichai ni kinga dhidi ya saratani. Tafiti mbalimbali zimeonyesha kuwa kwenye kila gram 100 ya mchaichai, kuna viondosha sumu ambavyo vina uwezo wa kuukinda mwili dhidi ya ugonjwa wa saratani. Mwaka 2006, timu ya watafiti kutoka Chuo kikuu cha Gurion, Israel waligundua mchaichai una uwezo wa kuua seli zinaweza kusababisha saratani. 2. Hutibu magonjwa ya kuhara. Husaidia umeng’enyaji wa chakula Chai ya mchaichai hurahisisha utaratibu wa mmeng’enyo wa chakula na pia hutibu magonjwa ya kuhara na maumivu ya tumbo ikiwamo kujaa gesi. Hurahisisha utaratibu wa kuondoa uchafu mwilini Katika matibabu, unatibu magonjwa mengi ikiwemo kushusha joto, hasa kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na malaria kali. 3. Husaidia kusafisha figo na mkojo. Mchaichai pia una kazi ya kusafisha figo ambayo kazi yake kubwa ni kusafisha damu mwilini, kuondoa mafuta mabaya mwilini ambayo mengi yanatengenezwa na kemikali kiwandani na hivyo mwili kushind

MAGAZETI YA LEO 16/12/2018

Image

Naibu Waziri aiagiza Tanesco kufikisha umeme Vituo 300 vya afya nchini

Image
Naibu waziri wa nishati Subira Mgalu katika kuumga mkono Juhudi za Rais Dk . John Pombe Magufuli ya kuboresha sekta ya afya hapa nchini ameliagiza Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) kuhakikisha wanapeleka miundombinu ya nishati ya umeme haraka iwezekanavyo katika maeneo ya vituo vipya vya afya 300 pamoja na hospitali 69 ambazo zinajengwa na serikali kwa lengo la kuboresha huduma ya matibabu kwa wananchi wake. Mgalu ambaye pia ni Mbunge wa viti maalumu kupitia Mkoa wa Pwani alitoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kutembelea miradi mbali mbali ya maendeleo iliyopo katika halmashauri ya mji Kibaha pamoja na kukagua mwenendo wa ujenzi wa upanuzi katika kituo cha afya mkoani kilichopo Wilayani Kibaha. “Kwa kweli nia ya serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inafikisha kwa haraka miundombinu ya umeme katika vituo vipya vya afya ambavyo vinajengwa pamoja na hospitali hivyo nachukua nafasi hii kuwaagiza Tanesco pamoja na REA kufikisha umeme haraka iweze

TACRI yatoa neema Butiama

Image
Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania (TaCRI) imefufua zao la kahawa wilayani Butiama mkoani Mara kwa kuanzisha vikundi vya wakulima baada ya zao hilo kutelekezwa kwa zaidi ya miaka 20 kutokana na ukosefu wa soko. Hayo yameelezwa na Meneja wa Kanda wa Kituo cha TaCRI kilichopo Sirari wilayani Tarime, Almas Hamad akikabidhi  vifaa mbalimbali kwa ajili ya kilimo pamoja na mbegu kilo 5 za kahawa aina ya Chotala ili kuziotesha zitakazozalisha miche 25,000 kwa kikundi cha shamba darasa(SHADABI) kijiji cha Biatika kata ya Buhemba wilayani humo, alisema kuwa lengo ni kuwawezesha wakulima kujipatia kipato kitokanacho na kahawa. ‘’Tumeamua kufufua zao hili  wilaya ya Butiama,Serengeti na Rorya lililokuwa likilimwa miaka ya nyuma lakini likaachwa kutokana na sababu za ukosefu wa elimu ya kilimo bora na masoko, tutaanza na vikundi 5 hapa Butiama,Serengeti kipo kimoja na Rorya kimoja na kadri tunavyokwenda vikundi vitaongezeka’’alisema Hamad. Aliongeza’’Tarime zao hilo limepig

Dk Kigwangalla ashusha makubwa

Image
Anna Potinus – Dar es salaam Neema imewashukia wasanii nchini baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii,Dk Hamisi Kigwangala kutoa ofa kwa wasanii wanaotaka kuandaa video za filamu ama za nyimbo zao katika maeneo ya utalii, kumuona yeye mwenyewe ili awape kibali cha kutumia vivutio hivyo vya utalii. Kigwangala ameyasema hayo leo Desemba 15, 2018 katika uzinduzi wa chaneli ya Utalii iliyopewa jina la Tanzania Safari uliofanyika ofisi za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) jijini Dar es salaam. Dk Kigwangala amesema anafanya hivyo ili kukwepa urasimu mkubwa wanaopata wasanii wanapoomba kufanyia filamu ama video zao kwenye maeneo ya utalii nchini. “Kila siku watanzania wanalalamika kuzuiwa kupiga picha katika baadhi ya maeneo na sasa hivi nimetoa ofa kwa wasanii wote wanaotaka kutengeneza video zao katika maene ya utalii wanione mimi moja kwa moja nitawapa vibali ili nawao watangaze vivutio vyetu,” amesema Aidha amewatoa hofu watanzania wanaodhani Wizara ya y

JPM afyekelea mbali maelekezo mapya wimbo wa taifa, bendera

Image
Mwandishi Wetu,  Dar es Salaam Rais Dk. John Magufuli, ameagiza bendera, nembo na wimbo wa taifa viendelee kutumika kama awali na kufuta maelekezo yalitolewa na Wizara ya  Elimu, Sayansi na Teknolojia, katika barua yake iliyoelekezwa kwa vyuo na taasisi za serikali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, leo Ijumaa Desemba 14, barua hiyo imetoa maelezo ambayo yanaathiri uzalendo wa Watanzania na imeleta mkanganyiko wa tafsiri ya rangi na alama zilizomo katika bendera ya taifa. “Hata mimi mwenyewe tangu nasoma shule hadi leo nafahamu kuwa Bendera ya Taifa ina rangi ya njano na si rangi ya dhahabu na rangi hiyo ya njano inawakilisha madini yote, sio dhahabu peke yake. “Kwa hiyo nimeamua kufuta barua kama kuna mabadiliko basi ni lazima yafanyike kwa kuzingatia taratibu zote kwa kuwa jambo hili ni la kitaifa, si la mtu mmoja,” ilisema taarifa hiyo. Aidha, Rais Magufuli ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kuwa wazalendo, kupenda nc

Upepo waharibu nyumba 150

Image
Hadija Omary, Lindi                                       Nyumba 157 yakiwamo majengo ya serikali zimebomolewa na upepo mkali ulioambatana na mvua iliyonyesha juzi Wilaya ya Nachingwea, mkoani Lindi. Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Rukia Muwango amesema mvua hiyo iliyoanza saa 10:30-11:30 jioni iliambatana naupepo mkali ambao licha ya kuharibu nyumba za kuishi katika kata za Nachingwea, Songambele na Stesheni, pia umeharibu Zahanati ya Stesheni. Ametaja maeneo yaliyokumbwa na upepo huo katika Kata za Stesheni kuwa ni nyumba na zahanati jumla 83, Kata ya Songambele nyumba 14na kata ya Nachingwea nyumba 60 na kufanya idadi kufikia 157. “Katika tukio hilo watu wanne wamejeruhiwa kwa kuangukiwa na kuta za nyumba zao, kisha kukimbizwa hospitali ya wilaya hiyo wakatibiwa na kuruhusiwa kurejea majumbani mwao, hakuna aliyepoteza maisha. “Hata hivyo, bado haijafahamika hasara iliyopatikana na ofisi yake imewaagiza wataalamu kufanya upembuzi yakinifu ilikubaini thamani