Grace Mugabe kukamatwa kisa hiki
Hatua hiyo imekuja baada ya mahakama kuibatilisha kinga yake ya kidiplomasia mwezi Julai.
Serikali ya Afrika Kusini ilikosolewa kwa kuruhusu Bibi Mugabe kuondoka nchini humo baada ya mashambulizi.
Gabriella Engels alimshutumu kwa kumpiga katika chumba cha hoteli mjini Johannesburg.
Msemaji wa polisi,Vishnu Naidoo amesema ''Siwezi kuthibitisha kuwa hati ya kumkamata Grace Mugabe ilitolewa Alhamisi iliyopita''.
Alisema polisi wanatafuta usaidizi kutoka idara ya Interpol kufanyia kazi waranti hiyo.
Haijafahamika kwa nini ripoti kuhusu waranti hiyo ilicheleweshwa na hakuna tamko lolote lililotolewa na Bibi Mugabe au mamlaka za Zimbabwe.
Familia ya Mugabe inamiliki mali nchini Afrika Kusini
Tukio la mashambulizi dhidi ya mwanamitindo lilitokea miezi mitatu kabla jeshi halijachukua mamlaka nchini Zimbabwe, hatua iliyomfanya Mugabe kujiuzulu baada ya kuwa madarakani kwa miaka 37.
Comments