Posts

Showing posts from January 20, 2019

Mahakama ya DR Congo yaidhinisha ushindi wa Felix Tshisekedi, Fayulu aitisha maandamano

Image
Mahakama ya katiba DR Congo imemuidhinisha rasmi Felix Tshisekedi kuwa rais wa nchi hiyo. Mgombea aliyechukua nafasi ya pili katika matokeo ya uchaguzi wa urais nchini DR Congo Martin Fayulu ameitaka jamii ya kimataifa kutotambua matokeo hayo na ameitisha maandamano. Taarifa yake inajiri baada ya ya mahakama ya kikatiba kuidhinisha ushindi wa mgombea mwengine wa upinzani , Felix Tshisekedi . Muungano wa Afrika ulisema siku ya Ijumaa kwamba kulikuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu matokeo hayo na kutaka matokeo rasmi kucheleweshwa. Bwana fayulu sio mgombea pekee ambaye anaamini kwamba yeye ni muathiriwa wa wizi wa kura huku data ilioibwa ikionyesha kuwa alipata kura mara tatu ya kura alizopata Tshisekedi. Haijulikani iwapo raia wataheshimu wito wa Fayulu wa kufanya maandamano. Siku ya Jumatatu ujumbe wa AU unatarajiwa Kinshasa na unatarajiwa kukutana na mtu anayedaiwa 'kuiba' kura rais anayeondoka madarakani Joseph Kabila. Iwapo Tshisekedi ataapishwa , muungano

Ndugai Tundu Lissu, ‘Unatakiwa urudi haraka’

Image
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amemtaka Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu kurejea nyumbani kwa kuwa hana kibali cha kuwa nje ya nchi. Ndugai amesema kuwa hawezi kumpangia Lissu mambo ya kusema ila ajue hana kibali cha kuendelea kuwa nje ya nchi wakati ofisi ya Spika haina taarifa. “Yeye ametoka kuugua aache uzushi arudi nyumbani, tunamsubiri nyumbani, kitu muhimu ni kwamba ajue hana ruhusa ya Spika ya kuwa huko anakozurura, sasa achunge kidogo, maana Spika ana nguvu zake, asimpe sababu,”amesema Ndugai. Aidha, Lissu ambaye amepona majeraha aliyopata baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 na watu wasiojulikana mwaka juzi, amedai kigezo kinachotaka kutumika kumvua ubunge ni utoro bungeni, ametoa waraka aliouita ‘Baada ya risasi kushindwa, sasa wanataka kunivua Ubunge’. Aidha, Lissu ameandika kwenye ukurasa wake wa kijamii kuwa, ”Ni taarifa gani ya maandishi watu hawa wanahitaji wakati nilishambuliwa nikiwa kwenye vikao

HABARI KUBWA LEO JUMATATU 21/1/2019

Image