Posts
Showing posts from January 14, 2019
Mbunge kuwasilisha hoja binafsi lugha ya kufundishia
- Get link
- X
- Other Apps
By
Maguruacademy
-
TIGANYA VINCENT, TABORA MBUNGE wa Tabora Kaskazini, Almas Maige (CCM), amesema wakati umefika kwa Watanzania kuanza kutumia Kiswahili kwa ajili ya kufundishia katika shule za sekondari na elimu ya juu kwa masomo yote. Amesema hatua hiyo itasaidia kuwawezesha vijana wengine kuelewa wanachofundishwa na kuwa na ufanisi katika utendaji kazi. Maige alisema hayo jana mjini Tabora alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu hoja yake aliyoiwasilisha bungeni kutaka Kiswahili kitumike kama lugha ya kifundishia na kujifunza katika shule za sekondari na vyuo nchini. Alisema utafiti uliofanywa na wataalamu na wanazuoni mbalimbali umeonyesha asilimia 50 ya wanafunzi hawaelewi wanachofundishwa kutokana na matumizi ya Kiingereza. Maige alisema hata wanavyuo vya ufundi wanaofundishwa kwa Kiingereza wanapomaliza masomo yao wanapokuwa kazini hawatumii lugha hiyo katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku bali wanatumia Kiswa...