MARA:Matokeo ya vinasaba ajali ya tarime yatangazwa

Hatimaye mili ya watu 11 kati ya 15 waliofariki katika ajali iliyohusisha  Magari mawili ya abiria na kusababisha vifo katika kijiji cha komaswa wilayani Tarime  Mkoani Mara na  kushindwa kutambuliwa, imetambuliwa  kupitia vinasaba huku mili mingine minne ikishindwa kutambuliwa kabisa.

Ajali hiyo ilitokea Novemba 26,2018 baada ya magari hayo kugogana uso kwa uso kisha kuwaka moto na kusababisha watu kuungua na mili yao kushindwa kutambulika hatua iliyopeleka serikali kuamua kuzika eneo la pamoja,na kufanya uchunguzi wa vinasaba ili kuweza kuwatambua.

Akitoa taarifa hiyo mkoani humo mkuu wa Mkoa wa mara Adamu Malima  amesema baada ya miili hiyo 11 kutambuliwa serikali ya mkoa imepanga kwenda kuweka vibao vyenye majina ya marehemu  Decenba 23  sambamba na ujenzi wa mnara.

Malima amesema kuwa serikali haitamzuia ndugu wa marehemu ambao watataka kuchukua mili ya wapendwa wao baada ya kutambuliwa kwaajili mazishi kwa taraibu za kimila na kidini kulingana na imani zao ambapo amesema watatakiwa taratibu za ufukuaji wa mili ikiwemo kuapata kibali cha mahakama.pia

Katika ajali hiyo jumla ya watu 17 walifariki Dunia ambapo 15 walifariki papo hapo  na wengine watatu wakiokolewa ambapo mmoja alifariki akiwa njiani kupelekwa hospital na mmoja alifariki hospital ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza akipatiwa matibabu.

Comments

Popular posts from this blog

Wanakijiji watishia kumburuza kortini DC

TMA yatoa tahadhari mafuriko yaja