Posts

Showing posts from December 19, 2018

Wanakijiji watishia kumburuza kortini DC

Image
Wanakijiji watishia kumburuza kortini DC Na Upendo Mosha-Moshi MKUU wa Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Kippi Warioba, ametuhumiwa na wananchiwa Kijiji cha Chekereni Weruweru, Kata ya Kindi kuvamia na kuvunja ofisi ya kijijihicho na kuchukua nyaraka mbalimbali. Kutokanana hali hiyo wananchi hao wametishia kumfikisha mahakamani kwa madai ya kuvunja kufuli la ofisi ya kijiji na kuchukua nyaraka hizo. Mwenyekiti wa kijiji hicho, John Bosco, aliyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana kijijini hapo. Bosco alisema kiongozi huyo amekuwa ni sehemu ya kuchochea migogoro na kwamba hawapotayari kuchonganishwa bali watafuata sheria. Alisema mgogoro huo ulianza baada ya mkuu huyo wa wilaya, kutumia nguvu nakuwanyang’anya kijiji ofisi yake na kukipa Chama Cha Mapinduzi (CCM) jambo ambalo ndio chanzo cha mgogoro huo. “Tunataka mahakama itafsiri kuwa ofisi ya Kijiji cha Chekereni Weruweru ni mali ya Serikaliya kijiji au CCM… mk

Shehena ya mizigo bandarini yaongezeka

Image
SHEHENA mchanganyiko katika Bandari ya Dar es Salaam zimeongezeka na kufikia tani milioni 3.2 ikilinganishwa na tani milioni 2.9 katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2018/2019. Bandari hiyo ina uwezo wa kuhudumia shehena tanimilioni 13.5, lakini mwaka 2017/2018 ilihudumia tani milioni 16.4 hatua iliyosababisha kufanya upanuzi kwa lengo la kuiongezea uwezo wa kuhudumia mzigomkubwa zaidi. Akizungumza juzi, Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Fred Liundi, alisema mafanikio hayo yanatokana na maboresho yanayoendelea ili kuhakikisha huduma zinatolewa kwa ufanisi. Kwa upande wa makontena, alisema walihudumia 184,200 juu ya lengo la makontena 154,171 ikiwa ni ongezeko la makontena 26,971. Kiasi kilichohudumiwa mwaka uliopita katika kipindi kama hicho ni makontena 169,974. “Yako masoko yanayohudumiwa na Bandari ya Dar es Salaam kama Zambia, DRC, Burundi, Rwanda na Uganda na tumehudumia asilimia 81.2 ya mizigo inayopitia bahari kuu kwenda katika nchi hizo,” alis

VIDEO: Rais Magufuli aendelee kuwatumbua, hawana faida - Jackline Wolper

Image
bonyeza hapa upate video

Mama wa watoto nane aamua kugombea urais DRC

Image
Zimebaki siku nne kwa raia wa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) kumchagua mtu atakayerithi mikoba ya Joseph Kabila. Wagombea watatu ndio wanaotajwa zaidi na ni vigumu hata kudhani kuwa wanaowania kiti hicho wapo zaidi ya ishirini na mmoja wao ni mwanamke. Bi Marie-Josee Ifoku yupo kwenye kinyang'anyiro cha kurithi Ikulu ya Kinshasa kutoka kwa Kabila akichuana na Emmanuel Ramazani, Martin Fayulu na Felix Tshisekedi ambao ndio wanaouvuma zaidi. Bi Ifoku, mwenye miaka 53 ni mama wa watoto nane si mgeni katika siasa. Alishawahi kuwa naibu gavana wa jimbo la Tshuapa kwa miezi sita mwaka 2016 kabla ya kuchaguliwa kuwa gavana wa jimbo hilo kuanzia Oktoba 2016 mpaka Oktoba 2017. Mwandishi wa BBC Swahili Mbelechi Msochi amefanya mahojiano na bi Ifoku hivi karibuni na amemueleza mipango yake endapo Wakongomani watampa ridhaa ya kuwaongoza. Bi Ifoku anasema kipaumbele chake cha kwanza kitakuwa kufanya mabadiliko ya katiba ili kuhakikisha haki za kiraia zinalindwa na nj

Mourinho aacha deni hili Manchester United

Image
Aliyekuwa Kocha wa Manchester United Jose Mourinho hatakuwa na shida ya kuuza nyumba kwa kuwa muda wote aliishi hotelini kama vile machale yalimcheza. Mourinho ameishi katika jiji la Manchester kwa muda wa siku 895, alikuwa akiishi katika hotel ya Lowry iliyopo jijini humo. Kwa siku hizo alizoishi hotelini hapo, Mourinho ameacha deni la pauni 537,000 (zaidi ya Sh bilioni 1.5), ambazo zitalipwa na Manchester United. Aliwasili katika hotel hiyo Julai 6, 2016 kabla ya kufukuzwa na kuondoka katika hotel hiyo Desemba 2018. Mkewe amekuwa akiishi jijini London na mwanaye wa kike, Matilde amehitimu chuo kikuu cha London na mtoto wake wa kiume, Jose Mourinho Jr alikuwa akiichezea timu ya vijana ya Fulham hadi Aprili 2017.

Shirika la ndege la Fastjet laamua kuingiza ndege mbili

Image
Akizungumza leo Jumatano Desemba 19, 2018 katika kipindi cha 360 kinachorushwa na Clouds Televisheni, Masha amesema  ndege ya shirika hilo aina ya Boeing 737 ambayo ilizuiliwa kuruka na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kutokana na hitilafu za kiufundi, sasa iko imara. “Kuanzia Jumamosi tukakuwa na ndege mbili aina ya Boeing 737 (pamoja na iliyopo sasa) ambazo zitakuwa tayari kufanya kazi. Hii  itasaidia kuondoa kero ya kusitishwa kwa safari,” amesema Masha. “Ndege zote zitakuwa na usajili wa Tanzania na kutokana na mahitaji na msimu,  hivi karibuni tunaweza kuongeza ndege nyingine moja au mbili aina ya Bombardier.” Amesema ana imani shirika litainuka na kuwa imara zaidi na juhudi zinazofanyika sasa ni kuzungumza na mamlaka ili kuwaruhusu kuanza kuuza tiketi. Amesema tayari baadhi ya matakwa ya mamlaka hiyo yametimizwa au kujibiwa ingawa bado mazungumzo yanaendelea. “Tunatarajia kurejesha safari zetu za Nairobi na Afrika Kusini kuanzia Februari 2018 na kua

Maalim seif asema: Nitaheshimu maamuzi ya mahakama

Image
Chama cha wananchi cuf kimesema kitaheshimu maamuzi yatakayo tolewa na mahakama kuu kuhusu khatma ya kesi zinazoikabili chama hicho ambazo zitatolewa uwamuzi wake mapema mwakani. Kesi hizo zinazoikabili chama hicho ni kesi inayohusu msajili wa vyama vya siasa na uruzuku ambayo kesi hiyo  itatolewa maamuzi yeke Januari 15 mwakani na kesi kuhusu kuwepo kwa bodi mbili ya wadhamini ndani ya chama hicho ambayo itatolewa uwamuzi wake February 18 mwakani. Kauli hiyo imetolewa Juzi na katibu mkuu wa chama hicho Maalim Seif Sharif hamadi wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kikao cha siku buli 16 hadi 28 decembar kilichiojadilihali ya kisiasa nchini, Maalim Seif alisema chama chake kina uamini muhimili wa mahakama  hivyo maaamuzi yoyote yataayo tolewa wao wamejidhatiti kuweza kuyapokea bila ya kipingamizi cha  aina yoyote. “maamuzi yoyote yatakayo tolewa sisi na mahakama sisi tumedhitatiti kuweza kuayapokea bila ya kipingamizi ya aina yoyote” alise

Angeline Mabula athibitisha wananchi kupokea zaidi ya Bilioni 1 kutoka Chuo cha Mzumbe

Image
Naibu Waziri wa Ardhi Maendeleo na Makazi, Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dk. Angeline Mabula, amethibitisha kulipwa fidia ya  Bilioni Moja na Milioni Mia Nne kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe kwa Wananchi wa Kata ya Sangabuye katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza. Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya  hafla fupi ya shukrani kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe, Mabula amesema kuwa wananchi 130 tayari wamepokea fidia iliyotoka na kwa sasa wako tayari kutoa ushirikiano kwa ajili ya kushirikiana nao katika ujenzi wa Tawi la chuo hicho ambapo eneo hilo lina ukubwa wa Hekari 220.

SMZ yataka vyuo vikuu nchini kuandaa mitaala ya elimu inayoenda na fursa zilizopo

Image
Makamo wa Rais wa Zanzibar,Balozi Seif Ali Iddi Amesema vyuo  vikuu vilivyopo zanzibar vinapaswa  kufuata mitaala ya elimu ambayo inaenda sambamba na mahitaji  pamoja fursa mbali mbali zilizopo nchini. Alisema ni lazima vyuo vikuu hivyo vikafanya kazi pamoja na Kamisheni ya mipango ya Zanzibar inayosimamia mipango ili iwe rahisi kupata vipaumbele na maeneo ambayo yanawekewa umuhimu. Alitoa mfano baadhi ya maeneo na vipaumbele vya umuhimu kwa taifa kama vmiradi mipya inayotarajiwa kuanzishwa Visiwani Zanzibar ya Mafuta na Gesi Asilia kufuatia Serikali ya Mapinduzi y Zanzibar kutiliana saini Mkataba  na Kampuni ya Rakgas ya Nchini Ras Al – Khaimah kuhusu mgawanyowa Rasilmali hiyo. Alisema Vyuo hivyo kwa sasa vina fursa ya kuchangamkia Miradi hiyo kwa kuanzisha mafunzo ya Mafuta na Gesi Asilia katika nganzi ya Diploma na Stashahada ili wakati utakapowadiua wa kuanza kwa Mradi huo Taifa lisijekuwa na upungufu wa Wataalamu. Alieleza kwamba Vyuo vikuu mahali popote pale Du

Rais Magufuli -Tunataka Tanzania iwe kama Ulaya

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa Watanzania wakiitunza amani ya nchi Tanzania itakuwa kama Ulaya. Rais Magufuli amesema hayo leo Disemba 18, 2018 alivyokuwa anahutubia kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la upanuzi wa Barabara ya Kimara-Kibaha yenye urefu wa kilometa 19.2. "Tunataka Tanzania tuitengeneze iwe kama Ulaya, na mimi nawaambia Watanzania tukishikamana vizuri tukaitunza amani yetu Tanzania itakuwa kama Ulaya kwasababu tuna kila kitu ila hizi resources zilikuwa zikipotea bure zikiibiwa kwasasa hivi kwa kipindi cha miaka mitatu miradi mingi mno ambayo inafanywa ni vigumu kuihesabu.

Nimetoka kwenye Chama kisichokuwa na shukurani mbele za Mungu - Waitara

Image
Mbunge wa Ukonga(CCM), Mwita Waitara amemwambia Rais John Magufuli kufanya kazi na kutosikiliza maneno ya watu. Naibu Waziri huyo wa Tamisemi ametoa kauli hiyo leo Jumatano Desemba 19, 2018 baada ya kupewa nafasi na Rais kuwasalimu wananchi katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi la upanuzi wa barabara ya Morogoro jijini Dar es Salaam iliyofanyika eneo la Kimara Stop Over. "Kwa mara ya kwanza nimesimama mbele yako Mh. Rais tangu nimeamua kutoka kwenye Chama kiukweli kabisa hakina shukurani mbele za Mungu, nikajiunga na Chama cha Mapinduzi," alisema Mwita Waitara.

Serikali yamfungia Diamond ndani, nje

Image
BARAZA la Sanaa la Taifa (Basata), limewafungia wanamuziki wa kizazi kipya, Nassib Abdul ‘Diamond Platinum’ na Raymond Mwakyusa, kufanya onyesho lolote ndani na nje ya nchi kwa muda usiojulikana pamoja na kukifuta kibali cha tamasha la ‘Wasafi Festival 2018’. Baraza hilo lilifikia uamuzi huo baada ya kugundua kuwa wasanii hao walikuwa wakidharau uamuzi uliotolewa na baraza hilo kwa kuendelea kuuimba wimbo wa ‘Mwanza’ ambao ulikuwa umefungiwa. Novemba 12 mwaka huu, Basata liliamua kuufungia wimbo huo kwa madai ya kuwa na mistari iliyokuwa ikikiuka maadili katika jamii. Taarifa ya Basata iliyotolewa jana ilieleza kuwa mbali ya kuwafungia wasanii hao, pia wamesitisha kibali cha tamasha la ‘WasafiFestival 2018’ baada ya kukiuka sheria za uendeshaji. “Baraza limefikia uamuzi huu kwa sababu ya wasani ihawa kuendelea kuonyesha dharau na utovu wa nidhamu kwa mamlaka zinazosimamia masuala ya sanaa nchini. “Pia kumekuwa na uvunjifu wa maadili uliokithiri unaofan

Dk. Magufuli umeingia kwenye historia

Image
WIKI kadhaa nchi yetu imeshuhudia inaingia kwenye historia baada ya Rais wetu, Dk. John Pombe Magufuli kusaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa umeme wa Bonde la Mto Rufiji kati ya Tanzania na Misri ambao umesubiriwa kwa zaidi ya miaka 40. Tukio hilo lililohudhuriwa na viongozi wote wa Kitaifa akiwamo Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na takriban mawaziri wote lilishuhudiwa pia na wananchi wote wa ndani na nje ya nchi kupitia vyombo vya habari. Ni chukue nafasi hii kumpongeza Rais Magufuli kwa uamuzi wabusara na wa dhati kuamua kuufufua mradi huu na kuuendelea ambao kwa maneno yake mwenyewe aliwaambia waliohudhuria hafla ya utiaji saini kwamba mradi huo ulianza tangu enzi za utawala wa Hayati Mwalimu Nyerere lakini ulikwama utekelezaji wake. Mradi wa umeme wa Bonge la Mto Rufiji si tu utawanufaisha Watanzania kwa maana ya kupungua kwa gharama za kununua umeme lakini pia mradihuo  utakuza uchumi wa Taifa letu kwa sababu utakapokam

Magufuli atoboa siri barabara za lami

Image
Rais John Magufuli, ametoa siri ya barabara za lami nchini kuwa ni waraka aliouwasilisha kwa Rais Benjamin Mkapa, mwaka 2001. Amesema waraka huo wa barabara wenye mapendekezo ulipitishwa na Rais Mkapa huku Baraza la Mawaziri likiukataa. Rais Magufuli mesema hayo leo Jumatano Desemba19, katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi la upanuzi wa Barabara ya Kimara-Kibaha ya Km 19. 2 yenye njia nane. “Mwaka 2001 kupitia Waraka wa Barabara uliowasilishwa na Waziri wa Ujenzi wakati huo tukapeleka mapendekezo kwenye Barazala Mawaziri, mapendekezo haya sikuyapitisha kwa Katibu Mkuu. “Wengi hamjui na ujanja niliofanya nilikwenda kumueleza Mkapa, akaniuliza watakubali mawaziri wenzako, akasema wewe ulete usiupeleke kwa makatibu, baadaye ikapelekwa kwenye Baraza la Mawaziri, wote wakaupinga,”amesema. Amesema waraka huo ulikuwa unasema itengwe Sh bilioni1.14 kwa ajili ya barabara akapewa amri Waziri wa Fedha wakati huo Basil Mramba akaanza kutenga fedha na barabara ya

JPM atekeleza ndoto ya mwaim JK nyerere

Image
MACHO ya Watanzania yameshuhudia historia kubwa ikiandikwa chini ya Rais Dk. John Magufuli baada ya kufanyika kwa tukio la utiaji saini mkataba wa ujenzi wa mradi wa umeme wa Bonde la Mto Rufiji kati ya Tanzania na Misri ambao umesubiriwa kwa zaidi ya miaka 40 sasa. Kabla ya kuendelea na makala haya nimpongeze Rais Dk. Magufuli kwa kuonesha uzalendo kwa nchi yake. Rais Dk. Magufuli amejiwekea historia kwa kuhakikisha mradi huo unafanikiwa. Hongera Rais. Baada ya kumpongeza Rais Magufuli nikiri kutambua kazi iliyopo mbele yetu katika kuhakikisha tunashirikiana kwa umoja wetu kufanikisha dhamira ya Rais wetu kuhakikisha Tanzania inakuwa na nishati ya umeme ambao utatosheleza mahitaji ya nchi yetu na hata kuuza kwa nchi nyingine. Kwa kukumbusha tu mradi huo uliosainiwa Ikulu jijini Dar es Salaam Desemba 13, mwaka huu ulishuhudiwa pia na Waziri Mkuu wa Misri, Dk. Mostafa Madbouly ambaye aliongozana na Waziri wa Nishati wa nchi hiyo, Dk. Mohamed Shaqqah pamoja na

Waliooana wakamatwe:mtaka asema

Image
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka, ameagiza kukamatwa mara moja wazazi wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Giyuki iliyoko kata ya Nkololo Wilayani Bariadi, ambao wanadaiwa kuoana baada ya kufanya mtihani wa darasa la saba mwaka huu. Kauli ya Mkuu huyo wa Mkoa imekuja baada ya Ofisa Elimu Utamaduni wa Mkoa, Charles Maganga, kuwasilisha taarifa ya kikosi kazi kilichoundwa kuchunguza chanzo cha Mkoa wa Simiyu kufanya vibaya katika matokeo ya darasa la saba mwaka 2018 kwenye kikao kilichofanyika leo mjini Bariadi. “Kufika leo jioni wawe wamekamtwa na watasherekea Sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya mahabusu, hili jambo siyo la kunyamazia lazima kama serikali tuchukue maamuzi, yanatusababishia kushuka kielimu,” amesema Mtaka. Katika taarifa hiyo Maganga amesema katika shule hiyo walibaini kuwa wazazi wa wanafunzi hao walikubaliana na kutoleana posa ili watoto wao waoane na baada ya kufanya mtihani harusi ya kufunga ndoa ilifanyika kijijini hapo. “Kwenye matokeo yao mvulana a

Serikali yaokoa mabilioni ya wagonjwa kutibiwa nje kupitia JKCI

Image
Serikali imefanikiwa kuokoa kiasi kikubwa cha fedha zilizokuwa zinatumika kupeleka wagonjwa wa moyo nje ya nchi kwa ajili ya upasuaji tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI). Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo wa JKCI,  Dk. Naiz Majani, amesema hayo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Jijini Dar es Salaam leo Jumatano Desemba 19. Dk. Majani amesema hadi sasa taasisi hiyo imewafanyia upasuaji wagonjwa wa moyo 1,040 ambapo kati yao, wagonjwa 600 wamefanyiwa operesheni kubwa na 400, upasuaji wa kawaida. “JKCI  imeweza kuokoa kiasi kikubwa cha fedha ambazo zilikua zinatumiwa na serikali kupeleka wagonjwa wa moyo nje ya nchi kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji,” amesema Dk. Majani. Aidha, amesema taasisi hiyo kwa kushirikiana na Taasisi ya ‘Save the Children’ wameanzisha mbio za ‘Heart Marathon’ kwa ajili ya kuhamasisha jamii kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza. Amesema mbio hizo zinatarajia kumalizika Desemba 28 mwa