Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli
ameweka Jiwe la Msingi Mradi wa Ujenzi Daraja Jipya na Barabara ya Aga
Khan Hadi Coco Beach.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine
wakipata maelezo toka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini
(TANROADS) Mhandisi Robert Mfugale kuhusu Mradi wa Ujenzi wa Daraja
Jipya la Selanderna Barabara unganishi ya Km 6.23 toka Hospitali ya Aga
Khan hadi ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es salaam leo Desemba 20, 2018
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipongezana na Balozi wa
Jamhuri ya Korea nchini Mhe. Cho Tae-ick baada ya kuweka jiwe la Msingi
la Mradi wa Ujenzi wa Daraja Jipya la Selander na Barabara unganishi ya
Km 6.23 toka Hospitali ya Aga Khan hadi ufukwe wa Coco Beach jijini Dar
es salaam leo Desemba 20, 2018. Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Mama
Janeth Magufuli na viongozi wengine wanashuhudia
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishirikiana na Balozi wa
Jamhuri ya Korea nchini Mhe. Cho Tae-ick kufunua pazia kuashiria
kuwekwa kwa jiwe la Msingi la Mradi wa Ujenzi wa Daraja Jipya la
Selander na Barabara unganishi ya Km 6.23 toka Hospitali ya Aga Khan
hadi ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es salaam leo Desemba 20, 2018.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Mama Janeth Magufuli na viongozi
wengine wanashuhudia
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea kwenye sherehe za
kuweka jiwe la Msingi Mradi wa Ujenzi wa Daraja Jipya la Selander na
Barabara unganishi ya Km 6.23 toka Hospitali ya Aga Khan hadi ufukwe wa
Coco Beach jijini Dar es salaam leo Desemba 20, 2018
Mchungaji wa Kanisa la Assemblies Of God maarufu kama ‘Mlima wa moto’ Dk Getrude Rwakatare, amemshukuru Rais Magufuli kwa kumgundua Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam. Mama Rwakatare amesema kuwa kwa mara ya kwanza alimuona Makonda ana bidii ya tofauti na jasiri. "Namshukuru Rais wetu kwa kumgundua Paul Makonda , mimi nakumbuka nilikumgundua akiwa kiongozi wa Wana vyuo pale Moshi alivyonialika kwenye mkutano mkubwa kabisa wa wana vyuo," alisema Mama Rwakatare. "Nilimuona ana bidii ya tofauti na ujasiri wa tofauti, niliona kwamba Mungu amempa wito ndani yake, nilikuiwa nasema Mungu naomba utokee mahali fulani kiwa bahati tukakutana tena kwenye Bunge la Katiba." Mama Rwakatare ameyasema hayo katika hafla ya viongozi wa dini iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda ya kupata chakula cha pamoja.
Comments