Wanaosambaza nyaraka za serikali bila idhini wapigwa marufuku
Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole
Nasha amesema ni kosa kusambaza nyaraka za serikali katika mitandao ya
kijamii bila idhini ya Mamlaka husika, hivyo ameagiza kuchukuliwa hatua
za kinidhamu na za kisheria kwa watumishi watakaobainika kusambaza
nyaraka hizo.
Naibu Waziri Ole Nasha ametoa agizo hilo mkoani Morogoro wakati akifunga semina ya mafunzo ya Huduma kwa Mteja na Utunzaji wa Kumbukumbu kwa baadhi ya Maafisa wa Wizara hiyo na kusisitiza kuwa hakuna mtumishi yeyote wa serikali asiyefahamu kuwa kutoa nyaraka za serikali bila idhini ni kosa la jinai.
“Kumekuwa na usambazaji wa nyaraka za serikali katika mitandao ya kijamii bila idhini na kwa bahati mbaya wakati mwingine unakuta nyaraka imewekwa mhuri wa siri lakini bado unaikuta huko, watumishi wa serikali lazima watambue kuwa kuna utaratibu wa kutoa nyaraka za serikali na kuna sheria ambazo zinawabana wale wote wanaotoa taarifa hizo bila kuidhinishwa”alisisitiza Naibu Waziri Ole Nasha.
Ole Nasha amewataka watumishi hao kutambua kuwa hakuna taasisi yeyote inayoweza kufanya kazi bila kuwa na kumbukumbu au nyaraka hivyo amewataka kuhakiksha utunzaji mzuri na salama wa nyaraka hizo kwani ni nguzo muhimu katika kufanikisha utendaji wa majukumu.
Mafunzo hayo yamefanyika kwa siku tano na yameshirikisha watumishi zaidi ya 50 kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Makao Makuu, Vyuo vya Ualimu vilivyopo Morogoro na baadhi ya watumishi kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA).

Comments