Maajabu! :Mwanafunzi mdogo alawiti watoto wenzake,polisi wamtafuta
Mwanafunzi wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi ya Wilunze mwenye umri wa miaka 14 anatuhumiwa kuwalawiti wanafunzi wenzake ambapo katika tukio la hivi karibuni alimlawiti mtoto wa miaka mitatu. Hayo yalibainishwa na Mtendaji wa Kijiji Cha Wilunze Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, Georgina Richard wakati akizungumza juzi katika mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji wa vijiji na kata kupitia mradi wa kutokomeza ukatili wa kijinsia, mimba na ndoa za utotoni unaotekelezwa na Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Woman Wake Up (WOWAP). Alieleza kuwa tukio la kulawitiwa mtoto wa kiume wa miaka mitatu lilitokea Novemba 26, mwaka huu kijijini hapo. Alisema mtuhumiwa huyo ni mtoro wa kudumu na mara ya mwisho alikuwa akisoma darasa la tatu Shule ya Msingi Wilunze. Alisema siku ya tukio mtuhumiwa huyo alimuingiza mtoto huyo kwenye nyumba ambayo haijamalizika na kumfanyia kitendo hicho. “Aliyeshuhudia kitendo hicho ndio alikwenda kutoa taarifa kwa mama wa mtoto ambapo...