SMZ yataka vyuo vikuu nchini kuandaa mitaala ya elimu inayoenda na fursa zilizopo

Makamo wa Rais wa Zanzibar,Balozi Seif Ali Iddi Amesema vyuo  vikuu vilivyopo zanzibar vinapaswa  kufuata mitaala ya elimu ambayo inaenda sambamba na mahitaji  pamoja fursa mbali mbali zilizopo nchini.

Alisema ni lazima vyuo vikuu hivyo vikafanya kazi pamoja na Kamisheni ya mipango ya Zanzibar inayosimamia mipango ili iwe rahisi kupata vipaumbele na maeneo ambayo yanawekewa umuhimu.

Alitoa mfano baadhi ya maeneo na vipaumbele vya umuhimu kwa taifa kama vmiradi mipya inayotarajiwa kuanzishwa Visiwani Zanzibar ya Mafuta na Gesi Asilia kufuatia Serikali ya Mapinduzi y Zanzibar kutiliana saini Mkataba  na Kampuni ya Rakgas ya Nchini Ras Al – Khaimah kuhusu mgawanyowa Rasilmali hiyo.

Alisema Vyuo hivyo kwa sasa vina fursa ya kuchangamkia Miradi hiyo kwa kuanzisha mafunzo ya Mafuta na Gesi Asilia katika nganzi ya Diploma na Stashahada ili wakati utakapowadiua wa kuanza kwa Mradi huo Taifa lisijekuwa na upungufu wa Wataalamu.

Alieleza kwamba Vyuo vikuu mahali popote pale Dunia ndivyo vyenye dhamana ya kutoa Wataalamu na Watafiti wa Fani mbali mbali ambao ndio chimbuko la  kuimarika kwa Uchumi unaopelekea kupunguza changamoto za ajira sambamba na kuongezeka kwa Pato la Taifa.

Hayo aliyabainisha wakati akisoma Hotuba kwa Niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dokta. Ali Mohamed sheini  wakati wa Mahafali ya 16 ya Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Zanzibar {ZU} kiliopo Tungu Mkoa wa Kusini Unguja,

 Balozi Akimwakilisha Rais alisema Uongozi wa Vyuo Vikuu vilivyopo Zanzibar vinapaswa kuzingatia Mitaala wanayofundishia Vyuoni iwapo  inakidhi mahitahi halisi ya fursa zinazoweza kuibua Wataalamu wa kutosha wa kulisaidia Taifa na Jamii katika Fani tofauti.

Alisema jamii hivi sasa inapita katika wakati wa mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia Duniani ambayo kwa vyovyote vile italazimika kujikita katika Elimu bora itayoweza kuwavusha salama katika mabadiliko hayo muhimu kwa maendeleo ya Uchumi na Taifa.

Hata hivyo Dr. Shein alielezea faraja na matumaini yake kutokana na jitihada kubwa zinazochukuliwa na baadhi ya Wawazi Nchini kuwaandaa Vijana wao kuingia katika kundi la Wanataaluma ambao mbali ya kuwajengea hatma yao na vizazi vyao lakini pia Taifa hufaidika kutokana na Elimu hiyo.

Alisema Wazazi hao mbali ya kutekeleza Wajibu wao katika misingi ya Imani ya Dini katika kuwawekeza Watoto wao katika Elimu lakini pia hawajatupa kwa kutumia fedha zao kwenye jambo hilo, Fedha ambazo walikuwa wanaweza kuzitumia kwa masuala mengine ya Kimaisha.

Mapema Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Zanzibar Tanguu {ZU}      Profesa Mustafa Roshash alisema Uongozi wa Chuo hicho kilichoasisiwa Mwaka 1998 umepata faraja kutokana na hamasa ya Jamii iliyojielekeza kupata Taaluma ya Elimu ya juu.

Profesa Mustafa Roshash alitoa wito kwa Wanataaluma wanaopitia elimu ya vyuo Vikuu kuendelea na mafunzo yao katika ngazi ya juu zaidi kwa kujielekeza kwenye tafiti kwa kadri ya fani zao walizobobea.

Alisema Uongozi wa Chuo hicho utaendelea kuimarisha Mitaala yake hadi kuona kila Mwanajamii anapata fursa ya kujiendeleza kwa kadri ya uwezo wake wa Kitaaluma.

Aliipongeza Wizara hya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kwa kuendelea kukiunga mkono chuo hicho katika Malengo yake ya kutoa Elimuy hapa Nchini na Ukanda wa Afrika Mahsriki kwa ujumla.

Akimkaribisha Mgeni rasmi katika Mahafali hayo ya 16 ya Chuo Kikuu cha Zanzibar {ZU} Waziri wa elimu na Mafunzo ya amali Zanzibar Mh. Riziki Pembe Juma aliuomba Uongozi wa Chuo hicho kufikiria kutumia Lugha ya Taifa katika Mahafali ya Mwaka ujao.

Mh. Riziki alisema hatua hiyo muhimu itawapa fursa Wanafunzi wa nje ya Zanzibar kuondoka na zawadi ya Lugha hiyo iliyopata umaarufa na kukubalika katika maeneo mbali mbali Duniani.

Jumla ya Wahitimu 1,076 wa Fani mbali mbali wamepata Vyeti, Diploma, Stashahadapamoja na Shahada baada yha kumaliza mafunzo yao kwa mujibu wa utaratibu wa Miaka yao.

Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunbguu {ZU} kilichoasisiwa mnamo Mwaka 1998 na kuanza kutoa Vyeti, Diploma na Stashahada na Shahada tayari kimeshazalisha wahitimu  9,344.

Comments

Popular posts from this blog

Wanakijiji watishia kumburuza kortini DC

TMA yatoa tahadhari mafuriko yaja