Nimetoka kwenye Chama kisichokuwa na shukurani mbele za Mungu - Waitara
Mbunge wa Ukonga(CCM), Mwita Waitara amemwambia Rais John Magufuli kufanya kazi na kutosikiliza maneno ya watu.
Naibu Waziri huyo wa Tamisemi ametoa kauli hiyo leo Jumatano Desemba 19, 2018 baada ya kupewa nafasi na Rais kuwasalimu wananchi katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi la upanuzi wa barabara ya Morogoro jijini Dar es Salaam iliyofanyika eneo la Kimara Stop Over.
"Kwa mara ya kwanza nimesimama mbele yako Mh. Rais tangu nimeamua kutoka kwenye Chama kiukweli kabisa hakina shukurani mbele za Mungu, nikajiunga na Chama cha Mapinduzi," alisema Mwita Waitara.
Comments