Posts

Showing posts from January 5, 2019

TAHARUKI: KANISA KATOLIKI LAANIKA HADHARANI JINA LA MSHINDI WA URAIS CONGO

Image
Baraza Kuu la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (Cenco), lenye ushawishi mkubwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, limesema linafahamu aliyeshinda uchaguzi wa rais ambao ulifanyika Desemba 30 mwaka jana na kuomba Tume ya Uchaguzi (CENI) kutangaza matokeo katika mazingira huru, haki na ukweli. Baraza hilo limetoa baada ya tume ya uchaguzi kutangaza kwamba italazimika kuchelewa kutangaza matokeo ya awali ya uchaguzi uliofanyika Jumapili iliyopita kutokana na hitilafu za kimitambo. Kanisa hilo limesema sampuli ya wawakilishi ilichapishwa katika vituo vya kupigia kura ambavyo vinawaruhusu kujua jina la rais aliyechaguliwa. Sampuli hiyo ni ya vituo zaidi ya 23,000 kati ya vituo 70,000 vilivyowekwa na Ceni nchini humo. Akizungumza na vyombo vya habari nchini humo, msemaji wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki, Padri Donatien Nshole, amesema si jukumu lao kutangaza matokeo, bali wao ni waangalizi lakini wanafahamu nani aliyechaguliwa na wananchi. “Ni muhimu kusisitiza kuwa k

WATANO WAGONGWA NA LORI WAKITOKA HARUSINI, WAFARIKI – VIDEO

Image
AJALI mbaya ya lori la mchanga lenya namba za usajili T155 ATC kugongana na gari la abiria aina ya Toyota Hiace imetokea majira ya saa 8 usiku wa kuamkia leo Jumamosi, Januari 5, 2019 katika maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar es Salaam ambapo lori hilo limeacha njia na kutumbukia mtaroni. Kutokana na taarifa ambazo hazijathibitishwa na Jeshi la Polisi, inadaiwa kuwa lori hilo liliigonga Hiace ikiwa imebeba watu wengi waliyokuwa wakitoka kwenye harusi na kusababisha vifo vya watu watano na wengine kujeruhiwa. =====

Uchaguzi DRC: Kanisa Katoliki lasema kuna mshindi wa wazi uchaguzi wa urais

Image
Serikali ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), imekemea ushawishi unaotolewa na kanisa Katoliki unaodai kuwa wanajua kiongozi aliyeshinda katika uchaguzi wa rais. Barnabe Kikaya Bin Karubi ambaye ni msemaji wa 'Common front for the Congo', ameiambia BBC kuwa "Jambo linalofanywa na kanisa ni kitu ambacho hakikubaliki, ni sawa na kuwaandaa watu kufanya mapinduzi". Serikali ya mseto imesisitiza kwamba ni Tume ya uchaguzi peke yake ndio inaweza kutangaza matokeo ya uchaguzi. Matokeo ya uchaguzi wa urais DRC 'kuchelewa' Huduma ya intaneti yafungwa DR Congo siku moja baada ya uchaguzi Wagombea wa upinzani walalamikia dosari uchaguzi DRC Kanisa Katoliki, ambalo lina ushawishi mkubwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, limesema kuwa kuna mshindi wazi wa urais katika uchaguzi uliofanyika Jumapili, kwa mujibu wa matokeo ambao wamefanikiwa kuyaona. Maaskofu wa kanisa hilo wamewataka watawala nchini humo kuwa wakweli na kutangaza matokeo hayo karib

MAGAZETI YA LEO 6/1/2019

Image