Posts

Showing posts from January 6, 2019

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Januari 7, 2019

Image
Fahamu yote yaliyojiri katika Magazeti ya Tanzania leo Januari 7, 2019. Hapa unapata habari zote zilizopewa uzito katika kurasa za mbele na kurasa za nyuma za habari za michezo na burudani.

MGOMO: Mrema awagumzo kwa wapinzani wenzake

Image
AZIZA MASOUD – Dar es Salaam MWENYEKITI wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustino Mrema, amesema hawezi kuungana na vyama vingine vya upinzani vilivyofungua kesi kupinga Muswada wa Sheria ya Vyama vya Siasa wa Mwaka 2018. Amesema anaamini kufanya hivyo hakuwezi kuondoa matatizo yaliyopo ambayo msingi wake unatokana na ubovu wa sheria zilizopo. Mrema ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja kupita baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kuanza kusikiliza kesi namba 31 ya kupinga muswada huo iliyofunguliwa mahakamani hapo Desemba 20 mwaka jana na viongozi wa vyama vya upinzani. Viongozi hao ni Kiongozi Mkuu ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, Kaimu Katibu Mkuu Cuf (Bara), Joram Bashange na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Umma wa chama hicho, Salim Bimani. Katika kesi hiyo mshtakiwa mkuu ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Dk. Adelardus Kilangi. Akizungumza na waandishi wa habari jana nyumbani kwake Salasala, Dar es Salaam, Mrema alisema wapinzani wanapaswa kufahamu kuwa hitaji la sasa

Makamu Mwenyekiti wa chama tawala Kenya ajiuzulu

Image
Makamu Mwenyekiti wa chama tawala cha Jubilee nchini Kenya, David Murathe amejiuzulu wadhifa wake huo. Lakini akanusha taarifa zilizojitokeza kwamba amejiondoa kwenye chama hicho.

Mlipuko wa bomu wauwa polisi mmoja

Image
Polisi mmoja ameuawa katika mlipuko karibu na kanisa mashariki mwa Cairo nchini Misri. Bomu lililotegwa kwa mikono karibu na Kanisa la Abu Seyfeyn huko Cairo lililipuka ghafla wakati polisi wakijaribu kulitegua na kusababisha kifo cha polisi mmoja. Polisi watatu wameripotiwa kujeruhiwa.

Tumbua tumbua: vigogo Ardhi Kigoma wavuliwa nyadhifa

Image
NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, Dk. Angelina Mabula amewavua nyadhifa wakuu wa Idara ya Ardhi katika Manispaa ya Kigoma Ujiji na Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao ya kazi ipasavyo. Waliovuliwa nyadhifa hizo ni Mkuu wa Idara ya Ardhi wa Manispaa ya Kigoma, Brown Nziku, Mkuu wa Idara ya Ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, Emanuel Magembe na Ofisa Ardhi Mteule, Paul Misuzi. Mabula alifanya uamuzi huo Januari 3, mwaka huu akiwa mkoani hapa baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Manispaa ya Kigoma Ujiji na Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma. Alifikia uamuzi huo baada ya watendaji hao kushindwa kusimamia maagizo na maelekezo yaliyotolewa tangu mwaka juzi kuhusu ukusanyaji wa kodi ya ardhi, uingizaji wa wamiliki wa viwanja na mashamba kwenye mfumo wa malipo kwa njia ya kielekroniki wa ardhi na utoaji wa hati za madai kwa wadaiwa sugu wa kodi ya ardhi. Mabula alisema pamoja na barua iliyoandikwa na Kamishna wa Ardhi Msaidiz