Posts

Showing posts from December 12, 2018

Buriani mradi wa Liganga na Mchuchuma By Mtanzania Digital - December 11, 2018

Image
Mwandishi Wetu ULE msemo kuwa chelewa chelewa utamkuta  mwana si wako  umejidhihirisha wazi kwenye suala lauwekezaji wa mradi wa Liganga na Mchuchuma wilayani Ludewa mkoani Njombe ambapo mwekezaji, Sichuan Hongda  Group yuko njia panda kwa kukosa mwelekeo na kuungwa mkono. Kampuni imesema madai yote yalikuwa na haki ya kujadiliwa kikamilifu na Serikali ambayo ilikwisha kutoa vyeti vya vibali vya madini na vishawishi vya uwekezaji. Sichuan Hongada Group inadai mradi umekuwa ukicheleweshwa na Serikali kutofanya yanayostahili huku ikijisahau  kuwa kampuni hiyo imekuwa ikibadilisha  masharti yake kama vile haijui nini inatakakwenye mradi. Wachunguzi wa mambo wanasema mradi huo kwa kila hali umepitwa na wakati kwani sheria zimebadilika na masharti yauchimbaji madini yameathiriwa kwa kiasi kikubwa na sheria mpya za Tanzania ambazo zimebadilika kudai kupata faida kwenyeutajiri wake. Hongda Group inashauriwa nayo kubadilika ilikuzu...

Wanawake viwandani Tanga wampa tano JPM utekelezaji sera ya viwanda

Image
Wanawake wanaofanya kazi viwandani mkoani Tanga, wamemshukuru Rais John Magufuli, kwa utekelezaji wa vitendo wa sera ya viwanda na kwamba uwepo wa viwanda ni mkombozi kwa mwanamke. Wakizungumza na Mtanzania Digital katika mahojiano maalumu katika Kiwanda cha Chokaa cha Neelkhanth Kilichopo JijiniTanga, baadhi ya wanawake kiwandani hapo wamesema utekelezaji wa sera ya viwanda unaofanywa na Rais magufuli ni mkombozi kwa mwanamke. “Kazi nyingi za viwandani zimekuwa zikifanywa na wanawake jambo linalowakwamua na umasikini kwani kupitia hiyo nimeweza kutunza familia,” amesema Mwanamvua Ramadhani, mfanyakazi katika kiwanda hicho. Amesema wanawake ambao hawana ujuzi pia wamepata fursa ya kupata ajira za muda mfupi katika viwanda mbalimbali nchini. “Kama unavyofahamu wanawake tuna majukumu mengi hivyo kwa kweli utekelezaji kwa vitendo sera hii ni mkombozi, mwanamke kwa sasa kukaa nyumbani na kulia njaa ni kujitakia tu,” amesema Mwanamvua. Kiwanda hicho ambach...

Miaka 50 ya Bakwata itumike kujitathmini

Image
DESEMBA 17, mwaka huu Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), linatarajia kufanya maadhimisho ya kutimiza miaka 50 tangukuanzishwa kwake. Maadhimisho hayo ya kitaifa ambayo yanatarajia kufanyika jijini Dar es Salaam, ni ya kwanza tangu baraza hilo lilipoanzishwa Desemba17, 1968 mkoani Iringa. Bakwata lilianzishwa kwa lengo la kuwaunganisha Waislamu wapate chombo cha kuwasemea, kuendeleza elimu kwa Waislamu, kutoa malezi namaadili mema kwa vijana, kuratibu shughuli zote za taasisi za Kiislamu nchini,kulinda na kusimamia mali za baraza hilo. Tangu lilipoanzishwa baraza hilo limeongozwa kwaawamu tatu, ambapo Sheikh Hemed Jumaa aliongoza kwa mara ya kwanza hadi mwaka2002, akafuatiwa na Issa Simba aliyedumu hadi mwaka 2015 na Sheikh Abubakar Zubeir aliyepo kwa sasa. Naamini kila uongozi uliopita unayo mambo mazuri uliyoyafanya kwa masilahi ya Waislamu wote nchini hususan awamu ya sasa chini ya Mufti Sheikh Zubeir ambaye tangu aingie madarakani ame...

Alichokisema Rais Magufuli mradi wa kuzalisha umeme

Image
Serikali ya Tanzania na Misri zimesaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme wa Stiegler’s Gorge ambao utakuwa na uwezo wa kuzalisha Megawati 2,100 za umeme. Mkataba huo umesainiwa leo Jumatano Desemba 12, Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo baada ya kusaini mkataba huo uliokuwa kati ya Rais John Magufuli na Waziri Mkuu wa Misri, Mostafa Madbouly, Watanzanaia wameombwa kuonesha ushirikiano wao kwa kuwa na mshikamano hadi hapo mradi huo utakapokamilika. “Niwaombe wananchi wanaoishi kwenye vyanzo vya maji muunge mkono mradii huu kwa kutunza vyanzo vya maji, msichome miti hovyo na kwa bahati nzuri Wakuu wa Mikoa wote mko hapa,” amesema Magufuli. Aidha, Rais Magufuli amesema mradi huo wa umeme wa Bonde la Mto Rufiji ulianza tangu kipindi cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, lakini kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo za kifedha nchi ilishindwa kutekelezajambo hilo.