Posts

Showing posts from December 17, 2018

Lukuvi, Makonda Wacharukia Migogoro ya Ardhi Gongo la Mboto

Image
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,William Lukuvi, yupo Mkoani Dar es Salaam akitatutua kero mbalimbali za wananchi wenye migogoro ya Ardhi , nyumba na masuala mbalimbali yanayohusu uvamizi wa nyumba. Lukuvi ameanza ziara yake leo katika Wilaya ya Ilala akiambatana na viongozi wa Mkoa akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema na Maafisa Ardhi wa Wilaya  ili kuweza kutatua kero zinazohusiana na masuala ya Ardhi na migogoro ya nyumba. Akiwa katika ziara yake hiyo kwenye viwanja vya Kampala vilivyopo Gongo la Mboto, Makonda amemwelezea Waziri Lukuvi jinsi ambavyo amekuwa akijitahidi kusikiliza kero za wananchi kuhusiana na migogoro ya Ardhi na kuwapatia elimu ya namna ya kumiliki Ardhi kwa kufuata sheria na kuwa na hati miliki ya eneo husika. Makonda amemhakikishia kuwa migogoro ya Ardhi katika mkoa wa Dar inaweza kupungua kama wananchi watafuta sheria na kanuni za Wizara ya Ardhi kama wakifuata taratibu zote...

Kanyasu aagiza tatizo la vinyago litatuliwe

Image
Mwandishi Wetu-Dar es Salaam BAADA ya malalamiko ya watalii wengi kulazimika kuacha vinyago viwanja vya ndege walivyokuwa wamevinunua katika maduka mbalimbali nchini kutokana na kukosekana kwa vibali kutoka Wakala wa Huduma za MisituTanzania (TFS), Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu ameuagiza wakala huo uangalie namna bora ya kutatua tatizo hilo kwa kuwa limekuwa na taswira mbaya kwa nchi. Alitoa kauli hiyo Dar es Salaam mwishoni mwa wiki alipozungumza na watumishi wa wakala huo makao makuu. Alisema watalii wengi hununua vinyago katika maduka mbalimbali kama zawadi ya kupeleka nchini kwao, lakini wanapofika viwanja vya ndege, hudaiwa vibali vya kuvisafirisha jambo ambalo huwalazimu kuviacha kutokana na usumbufu wanaoupata. Kanyasu alisema jambo hilo limekuwa likiwafanya watalii wengi kuondoka nchini wakiwa wamekasirishwa kutokana na utaratibu huo kutokuwa wazi, huku wakiamini wamedhulumiwa mali yao. “Malalamiko hayo si mazur...

Fastjet yasitisha safari zake, kurudisha nauli kwa abiria

Image
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam Kampuni ya Ndege ya Fastjet Tanzania imesitisha safari zake kwa muda usiojulikana kutokana na sababu za kiutendaji. Taarifa iliyotolewa na Fastjet leo Jumatatu Desemba 17, kampuni hiyo pia imetoa taarifa kwa wateja wake wote waliokata tiketi kwa ajili ya kusafiri kati ya Desemba mwaka huu na Januari mwakani watarudishiwa fedha zao na Menejimenti ya Fastjet. “Wateja wote watarudishiwa fedha zao za nauli kwa utaratibu walionunua kuanzia Desemba 20 mwaka huu pia makampuni na mashirika mbalimbali ambayo yalikuwa yanafanya biashara na fastjet yawasiliane nasi kupitia barua pepe au maofisa husika, tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza,” imesema taarifa hiyo.

Mshtakiwa adai Waziri Lukuvi alimpora begi la fedha

Image
Kulwa Mzee, Dar es Salaam Mkurugenzi wa Kiluwa Group, Mohammed Kiluwa amedai mahakamani kwamba Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, alimkaba akiwa ofisini kwake akimlazimisha kutoa hela alizo nazo kwenye mkoba na alipogoma waziri mwenyewe akafungua zipu akazitoa akaweka mezani na kisha akatoka nje na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wakaingia. Kiluwa amedai hayo leo saa tatu asubuhi katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala mbele ya Hakimu Mkazi Samweli Obas, akiongozwa na Wakili wake Imani Madega ambapo katika utetezi wake amedai alikuwa kwenye manunuzi ya vitu vya ofisi, walikuwa wanakarabati ofisi, alipanga kuanza kununua kwanza ndiyo aende ofisini kwa waziri lakini Waziri alimpigia simu mara tatu akimuharakisha aende ofisini kwake anamchelewesha ndipo alipokatiza kazi yake akaenda. Amedai waziri alitaka afike ofisini kwake akiwa na hati zake 57 lakini hakwenda nazo kwa madai kwamba mwenzake anayetunza alisafiri. ...

Kitakachojiri katika mabasi Des. 20

Image
LEONARD MANG’OHA-DAR ES SALAAM MABASI ya abiria yanayofanya safari kwenda mikoani na nchi jirani, yanatarajia kuanza safari saa 11:00 alfajiri katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka. Katibu Mkuu wa Chama cha Wamiliki Mabasi Tanzania (Taboa), Enea Mrutu aliliambia MTANZANIA jana kuwa hatua hiyo ilifikiwa katika kikao kati yao, Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) na Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani. Mrutu alisema utaratibu huo utayahusu mabasi yanayokwenda mikoa yote nchini isipokuwa katika maeneo yenye changamoto kubwaya kiusalama ikiwamo Kigoma, Sumbawanga na Rukwa. Alisema utaratibu huo utaanza kutekelezwa Desemba 20 mwaka huu, ambapo magari yote yaliyokuwa yakizuiwa Dodoma, Morogoro na Shinyanga sasa yataruhusiwa kutembea usiku ili yakamilishe safari. “Kwa mfano njia ya kati sehemu yenye changamoto ni kutoka Shinyanga kwenda Mwanza, hapo tumekubaliana uwekwe utaratibu kwamba kwa sababu magari ni meng...

Apandishwa kizimbani kwa unyang’anyi wa kutumia silaha

Image
AVELINE KITOMARY NA JOHN KIMWERI (DSJ) -DAR ES SALAAM MKAZI wa Kigogo Kati, KulwaAlly (33) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni mwishoni mwa wiki kwa shtaka la unyang’anyi wa kutumia silaha. Akisomewa shtaka hilo mbele ya hakimu Joyce Mushi, Mwendesha Mashtaka wa Jamhuri, Ramadhan Mkimboalidai kuwa Machi 30, mwaka huu eneo la Magomeni Morocco, Wilaya ya Kinondoni,Dar es Salaam, mshtakiwa alimtishia Mwinyipembe Waziri kwa panga na kuiba pikipiki aina ya Boxer yenye namba MC 538 yenye thamani ya Sh 2,360,000 mali yaFatuma Miraji. Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo, huku upande wa Jamhuri ukisema upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. Kutokana na kesi hiyo kutokuwa na dhamana mshtakiwa alirudishwa rumande hadi itakaposomwa Desemba 28,mwaka huu.

Historia imejirudia Simba SC imewashindwa Nkana FC

Image
Moja kati ya habari kubwa kwa upande wa soka leo nchini Tanzania ni pamoja na Bingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba SC kukubali kipigo cha magoli 2-1 dhidi ya Nkana FC ya Zambia katika game ya round ya kwanza ya CAF Champions League ilyochezwa mjini Kitwe Zambia. Kwa mujibu wa mwandishi wa habari za michezo wa Azam TV Zakazakazi, Simba SC imekuwa haina historia nzuri dhidi ya Nkana, hivyo kupoteza leo haikuwa mara ya kwanza kupoteza mchezo dhidi ya Nkana, naambiwa Simba leo imepoteza kwa mara ya tatu dhidi ya Nkana toka ipoteza mara mbili tofauti na kutolewa mwaka 1994 robo fainali na mara ya pili 2002 hatua ya mtoano kama hii. Moja kati ya habari kubwa kwa upande wa soka leo nchini Tanzania ni pamoja na Bingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba SC kukubali kipigo cha magoli 2-1 dhidi ya Nkana FC ya Zambia katika game ya round ya kwanza ya CAF Champions League ilyochezwa mjini Kitwe Zambia. Kwa mujibu wa mwandishi wa...

Fata Kanuni hizi za Kilimo bora cha Tangawizi uvune zaidi

Image
Tangawizi hutumika kama kiungo katika kuongeza ladha, harufu na kuchangamsha katika vinywaji (kama chai, soda, juisi, vilevi n.k) na vyakula mbalimbali kama mikate, biskuti, keki, nyama za kusaga, achari n.k. Hutumika pia katika viwanda vinavyotengeneza madawa ya tiba mbalimbali kama dawa za meno, kikohozi, tumbo na muwasho wa ngozi n.k. pia hutumika katika vipodozi kama poda n.k).Asili ya zao hili ni maeneo ya kitropiki ya bara la Asia na hasa katika nchi za India na China. Zao hili linazalishwa kwa wingi kutoka katika nchi ya Jamaica. Hapa nchini zao hili hulimwa katika mikoa ya Kigoma, Tanga, Morogoro, Pwani, Mbeya na Kilimanjaro. Aina ya Tangawizi. Hakuna uthibitisho wa aina za tangawizi ambazo hulimwa hapa nchini ila kuna dalili ya kuwa na aina za White Africa (Jamaica) na Cochin (flint); hii huwa na tunguu ngumu zenye nyuzi. Tabia ya Mmea. Tangawizi ni mmea unaotambaa chini ya ardhi, wakati wa masika hutoa majani juu ya ardhi. Jamaica ina rangi hafifu ya kahawia...

Ilichokisema Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) juu ya mafuriko

Image
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari kwa wakazi wa baadhi ya mikoa nchini humo kutokana na vipindi vya mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha katika siku tano zijazo. Hayo yameelezwa jana Jumapili Desemba 16, 2018 katika  taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na mamlaka hiyo. TMA imewataka wakazi wa maeneo ya Kanda ya Ziwa, Kaskazini, Kusini na karibu na Bahari ya Hindi kuchukua tahadhali hiyo. Taarifa hiyo inaeleza kuwa kuanzia leo Jumatatu Desemba 17, 2018 hadi Desemba 20, 2018 baadhi ya mikoa itaathiriwa na mafuriko jambo ambalo litafanya baadhi ya shughuli za kijamii kusimama. “Hii inamaanisha kuwa mafuriko yatatokea katika maeneo mengi na kuathiri jamii nzima, kuvurugika kwa usafiri na barabara kubwa kutopitika, hatari kwa maisha kutokana na maji kujaa au yanayopita kwa kasi,” inaeleza.

Kwa nini ni msimu wa Liverpool EPL?

Image
IKIWA imetwaa mara 18 taji la Ligi Kuu England, Liverpool ni moja ya klabu ya soka yenye mafanikio makubwa zaidi nchini England. Hata hivyo, Wekundu hao walitwaa ubingwa wao wa mwisho wakati ikiitwa Ligi Daraja la Kwanza mwaka 1990, na bado hawajatwaa taji wakati ligi hiyo ilipobadilishwa na kuitwa Ligi Kuu. Makocha nane tofauti wamejaribu kumaliza ukame wa kutwaa taji hilo kwa Liverpool katika nyakati tofauti, lakini hakuna aliyeweza kufikia mafanikio. Walimaliza nafasi ya pili mara tatu, ukiwamo msimu wa hivi karibuni wa 2013-14. Hata hivyo, mambo yanaonekana kuwa mazuri kwao msimu huu, kwani wakiwa ndio timu pekee ambayo hadi sasa haijafungwa kwenye Ligi Kuu. Vijana hao wa kocha Jurgen Klopp kwa sasa wapo kileleni mwa msimamo mwa Ligi Kuu na pengine msimu huu anaweza kumaliza ukame huo. Hapa tunaangalia sababu tatu kwa nini Liverpool itatwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu. 3. Safu ya ushambuliaji isiyozuilika Liverpool ni moja ya timu yenye safu bora zaidi ya ush...

Meli zachangamsha biashara ya usafirishaji

Image
MELI za mizigo za MV Ruvuma na MV Njombe zimeongeza mwamko wa biashara, hasa usafirishaji makaa ya mawe katika bandari za Ziwa Nyasa. Makaa ya mawe husafirishwa kutoka Bandari ya Ndumbi wilayani Nyasa hadi katika Bandari ya Kiwira iliyopo wilayani Kyela. Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea bandari za Itungi na Kiwira juzi, Meneja wa bandari za Ziwa Nyasa, Abed Gallus alisema meli hizo zenye uwezo wa kubeba tani 1,000 kila moja zimegharimu Sh bilioni 11 na zilianza kutengenezwa mwaka 2015 na kukamilika mwaka jana. “Meli za mizigo na ujenzi wa meli ya abiria (MV Mbeya) ni miradi ya maendeleo tuliyoanza kuitekeleza mwaka 2015 ili kuongeza ufanisi wa bandari za Ziwa Nyasa. “Tunashukuru mwamko wa wateja umeanza kuwa mzuri, hasa wale wanaojihusisha na biashara ya makaa ya mawe,” alisema Gallus. Alisema meli hizo tayari zimeshafanya safari saba hadi sasa na kati ya hizo, nne zilikuwa za majaribio na tatu za kibiashara ambazo zilifanywa kati ya Se...