Posts

Showing posts from December 16, 2018

Yaliyo mkuta naibu Katibu Mkuu Chadema

Image
                RAYMOND MINJA-IRINGA NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) upande wa Zanzibar, Salumu Mwalimu, amekamatwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa. Mbali na Mwalimu, wengine waliokamatwa ni Katibu wa Chadema wa mkoa huo, Jakson Mnyawami na Mwenyekiti wa Bavicha Wilaya ya Mbeya, Jailos Mwaijande. Viongozi hao walikamatwa jana wakijiandaa kuingia kwenye kikao cha ndani wilayani Mufindi kwa lengo la kujadili uchaguzi wa ndani wa chama hicho. Ilidaiwa kuwa hatua ya kukamatwa kwa viongozi hao ilitokana na agizo la Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Jamuhuri William kwa kuwa ofisi yake haikuwa na taarifa ya kufanyika kwa kikao hicho. Akizungumza na MTANZANIA, mbunge wa Viti Maalumu Chadema, Suzan Mgonakulima, alisema wameshangazwa na kitendo cha Mkuu wa Wilaya ya Mufindi kutumia Jeshi la Polisi kuzuia mkutano wao wa ndani ambao uko kisheria. Alisema walipofika kwenye ukumbi ambao walitarajia kufanyia mkutano huo, walikuta a

Makubwa yawakumba Vigogo Tanesco

Image
Ni kutokana na katikakatika umeme MWANDISHI WETU WAZIRI wa Nishati, Dk. Medard Kalemani ameagiza kung’olewa kwa vigogo wawili wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kwa kile alichodai ni sababu ya uzembe. Mbali ya kung’olewa, Waziri Kalemani ameagiza vigogo wavuliwe nyadhifa zao zote na uchunguzi wa kina dhidi yao uanze mara moja. Dk. Kalemani alitoa maagizo hayo mbele ya Mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco, Dk. Alexander Kyaruzi. Akizungumza na waandishi wa habari Dodoma juzi, Dk. Kalemani aliwataja vigogo hao ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uzalishaji, Mhandisi Abdallah Ikwasi na Naibu Mkurugenzi Mtendaji Usambazaji,Mhandisi Kahitwa Bashaija. “Kwa hiyo kuanzia sasa bodii chukue hatua dhidi ya Naibu Mkurugenzi wa ‘Generation’ (uzalishaji umeme) na Naibu Mkurugenzi wa ‘Transmission’ (usambazaji umeme). “Bodi ichukue hatua za kiutawala ikiwa ni pamoja na kuwavua nyadhifa zao kuanzia leo (juzi) na uchunguzi wa kinaufanyike kwa mamlaka mliyonayo,” alisema. Dk. Kalemani alisema

Lundo la barua lamiminika Ikulu

Image
Na BENJAMIN MASESE – MWANZA OFISI ya Rais-Ikulu imesema inapokea malalamiko na barua nyingi kutoka kwa wananchi na watumishi wa umma yanayoshughulikiwa na Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu kitendo ambacho ni utovu wa nidhamu na ukiukwaji wa sheria. Akizungumza mjini hapa juzi kwa niaba ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi wa kati akifunga mkutano wa kazi wa siku mbili kwa makatibu tawala wasaidizi wa mkoa, makatibu tawala wilaya, wakuu wa idara ya utawala na rasilimali watu na wanasheria wa mamlaka za Serikali za Mitaa kutoka mikoa ya Geita, Kagera, Mara, Mwanza na Simiyu ofisa kutoka Ofisi ya Rais-Ikulu, Francis Mang’ira, alisema masuala mengi yanayofika Ikulu yalipaswa kushughulikiwa na ngazi za wilaya na mkoa. “Masuala mengi yanayofika Ikulu yalipaswa kushughulikiwa na ngazi zawilaya na mkoa, lakini yanavuka hadi ngazi za taifa ikiwa chanzo ni watumishikutotimiza wajibu ipasavyo huku baadhi yao hutumia akili binafsi na ubinafsijambo ambalo kiutumishi hali

Mke aongea Mumewe Sheikh kutekwa kwa siku ya tisa leo

Image
Leo December 14, 2018 Taarifa kutoka Shule ya Sekondari Islamiya iliyopo Nyakato Mwanza zinasema Mwalimu Mkuu kitengo cha Dini Sheikh Bashiru Habibu ametekwa kwa siku ya tisa leo na Watu wasiofahamika. AyoTV na  millardayo.com imezungumza na Mke wa Sheikh na kusimulia namna alivyopokea taarifa ya mume wake kutekwa kwa siku ya tisa leo. “Sisi tulipata taarifa siku ya tukio jioni na mpaka leo sijui Mume wangu alipo, ila alichukuliwa na gari akiwa eneo la Shule na lilikuwa halina namba” Mke wa Sheikh