Kamishna TRA ‘atangaza’ ajira kiaina
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Charles Kichere, amesema mamlaka hiyo ina upungufu wa rasilimali watu 1,930 hali inayosababisha ucheleweshwaji wa ukusanyaji kodi na kutofungua ofisi zao katika baadhi ya wilaya na kuifanya serikali kukosa mapato ya maeneo hayo. Kichere ameyasema hayo leo alipokuwa akiwasilisha taarifa ya TRA katika kikao cha Rais Dk John Magufuli na mamlaka hiyo na wakuu wa mikoa kilichofanyika leo Jumatatu Desemba 10, jijini Dar es Salaam ambapo amesema mbali na upungufu huo pia wanahitaji nyumba 114 za wafanyakazi wa mipakani na ukarabati wa majengo 76 ya ofisi zao ili kuwapa mazingira mazuri ya kufanya kazi zao kwa ufanisi na kuongeza mapato. Aidha, Kamishna Kichere pia ameiomba serikali kupitia upya mfumo wa ulipaji kodi kwa wafanyabiashara wadogo ili kuwasaidia kulipa kodi kwa hiari na kuwaandalia maeneo maalumu ya kufanyia biasha...