BENJAMIN MASESE MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Geita imehukumiwa Katibu wa Baraza la Kata la Nyamboge, Theleza Barnabas, kifungo cha miaka mitano au kulipa sh 200,000 kila kosa kwa kupatikana na hatia ya kuomba na kupokea rushwa. Alilipa faini na kuachiwa. Akitoa hukumu, Hakimu wa mahakama hiyo, Jovith Kato alisema mahakama ilizingatia ushahidi wa jamuhuri na ushahidi wa utetezi. Awali, Mwendesha Mashitaka wa Takukuru, Dennis Lekayo alidai Septemba 13, 2018 katika Kata ya Nyamboge wilayani Geita, mshitakiwa aliomba rushwa ya Sh 200,000 kutoka kwa Sanda Magohe amsaidie kupata ushindi kwenye shauri la ardhi namba 01/2018 dhidi ya Dotto Maonyole lilokuwa linasikilizwa na Baraza la Kata ya Nyamboge. Baada ya kuombwa rushwa hiyo, Sanda ambaye alikuwa ni mlalamikaji katika shauri hilo, aliamua kutoa taarifa hiyo kwa Takukuru Mkoa wa Geita ambako mtego uliandaliwa ...