Wawili kizimbani waponzwa na WhatsApp



Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ardhi, Anna Mwaisumo (23) na mpenzi wake Samson Kisuguta (28), wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka manne ikiwemo ya kulawiti na kusambaza picha za ngono kwenye mtandao wa kijamii wa WhatsApp.

Mwaisomo ambaye makazi yake ni kwenye Hosteli za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) huku Kisuguta ni mkazi wa Msasani na mfanyabiashara walifikishwa mahakamani hapo leo Ijumaa mbele ya Hakimu Mkazi, Salim Ally.

Wakili wa Serikali, Mwanaamina Kombakono akisaidiana na Janeth Magohe alidai kuwa washitakiwa hao walitenda makosa hayo kati ya mwaka 2017 na mwaka huu maeneo ya Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam.

Magohe alidai katika mashitaka ya kwanza kuwa, washitakiwa wote kwa pamoja katika tarehe na mahali kusikofahamika mwaka jana, ndani ya jiji hilo, walikula njama kutenda kosa la kulawiti, kuchapisha picha za ngono na kulazimisha kupata fedha ili kutochapisha picha hizo.

Alidai katika mashtaka ya pili kuwa, Disemba 10, mwaka jana maeneo ya Nyumba ya kulala wageni ya Morgan maeneo ya Msasani wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, Kisuguta alimlawiti kinyume na maumbile mwanafunzi mmoja wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT- jina linahifadhiwa). Katika mashitaka ya tatu,

Inadaiwa Oktoba 7, mwaka huu ndani ya jiji hilo, Mwaisomo pamoja na Kisuguta walichapisha picha za ngono kupitia ukurasa wa WhatsApp kinyume na sheria.

Pia alidai Novemba 13, mwaka huu, ndani ya jiji hilo, washitakiwa hao walimlazimisha mlalamikaji huyo kutoa fedha taslimu Sh 250,000 ili wasichapishe picha hizo.

Washitakiwa hao walikana mashitaka na upande wa mashitaka ulidai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika hivyo waliomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Ally alitaja masharti ya dhamana kuwa kila mshitakiwa atatakiwa kuwa na wadhamini wawili wenye barua za utambulisho kutoa serikali za mitaa watakaosaini dhamana ya Sh 500,000 kila mmoja.

Hata hivyo, washitakiwa hao walikosa dhamana baada ya kushindwa kutimiza masharti hayo na kurudishwa rumande hadi Januari 3, mwakani kesi itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.

Inadaiwa kuwa Mwaisumo alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mlalamikaji huyo wakati wakisoma sekondari ya juu na baada ya kuchaguliwa kujiunga na vyuo tofauti hawakuwa na mahusiano mazuri

Comments

Popular posts from this blog

Wanakijiji watishia kumburuza kortini DC

TMA yatoa tahadhari mafuriko yaja