Rais azitafuta fedha zilizojenga nyumba hewa


Ijumaa , 21st Dec , 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Maguful, amebainisha sababu za kufanya mabadiliko kwenye Jeshi la Magereza kuwa ni kutokana kutoa fedha ambazo aliagiza kujengwa kwa nyumba za maaskari lakini mpaka sasa hazijajengwa.

Rais Magufuli
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam wakati akizungumza kwenye hafla ya utoaji vyeo kwa wahitimu wa maofisa na Ukaguzi, ambapo ameshangazwa kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya askari magereza lakini hakuna iliyojengwa.
"Kule Magereza nilitoa pesa kwa ajili ya kujenga nyumba za askari magereza pale Ukonga, zile nyumba mpaka leo hazipo na hela zimeisha, ndiyo maana nilifanya mabadiliko haraka haraka pale".
"Niwaeleze ukweli huwa ninauvumilivu lakini uvumilivu wa kwenye fedha huwa unanishinda, unatoa nyumba kwa ajili ya maaskari lakini hakuna kinachojengwa, nimemuagiza Kamishna Magereza azifuatilie hizo fedha," amesema Rais Magufuli.
Aidha Rais Magufuli amemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini kuwapongeza maaskari ambao watakuwa wakitekeleza majukumu yao kwa mujibu wa taratibu zao ili kuinua morali ya maaskari hao.
Nilikwishaeleza kuwa sitaki kuona askari wangu anawekwa ndani wakati alikuwa anatekeleza wajibu wake, ninataka niwambie siku zote nitawatetea ninyi mumtangulize Mungu mbele katika kila mnachokifanya,” ameongeza.

Comments

Popular posts from this blog

Wanakijiji watishia kumburuza kortini DC

TMA yatoa tahadhari mafuriko yaja