Sirro-Tumejipanga uchaguzi wa 2020"-


Ijumaa , 21st Dec , 2018
Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon N. Sirro amesema Jeshi hilo limejipanga vya kutosha kusimamia usalama katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika na ule wa 2020.
                                                       
Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon N. Sirro.
Kamanda Sirro ameyasema hayo leo Disemba 21, 2018 katika mahafali ya kuhitimisha mafunzo ya maofisa na wakaguzi wasaidizi wa polisi, ambapo ameweka wazi kwamba hawatatoa nafasi kwa mtu yeyote kuhatarisha amani ya nchi ya Tanzania.
Tumejipanga vizuri kuhakikisha uchaguzi unakwenda vizuri. Siku zote huwa nasema kama unaamua kuchukua silaha ya AK 47 ambayo haipatikani duka lolote na kuingia nayo barabarani ili uwatishe wananchi, hatuwapi nafasi,” amesema.
Kwa kutilia mkazo kauli ya IGP Sirro, Rais Magufuli amelikumbusha Jeshi hilo kuhakikisha kunakuwa na usala wakati wa uchaguzi.
Ninawakumbusha jeshi la polisi kuwa tumebakisha siku chache kuingia mwaka 2019 ambao ni wa uchaguzi wa serikali za mitaa kama tunavyofahamu chaguzi nyingi zinaleta fujo hivyo mkasimamie na kuhakikisha kunakuwa na usalama," amesema Rais Magufuli.
Mbali na hayo, Rais Magufulia amelitaka jeshi la polisi kukiangalia kitengo cha fedha na kwamba yapo malalamiko mengi ikiwemo suala la fedha  zinazotumwa na serikali kutowafikia wahusika.
"Ninataka Jeshi la Polisi pamoja na majeshi mengine pasiwe na malalamiko lazima kila mmoja afaidike na uaskari wake,” Rais Magufuli.

Comments

Popular posts from this blog

Kitakachojiri katika mabasi Des. 20

DRC CONGO :UN YAVIMBIWA