Uchaguzi DRC: Kanisa Katoliki lasema kuna mshindi wa wazi uchaguzi wa urais

uchaguziSerikali ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), imekemea ushawishi unaotolewa na kanisa Katoliki unaodai kuwa wanajua kiongozi aliyeshinda katika uchaguzi wa rais.
Barnabe Kikaya Bin Karubi ambaye ni msemaji wa 'Common front for the Congo', ameiambia BBC kuwa "Jambo linalofanywa na kanisa ni kitu ambacho hakikubaliki, ni sawa na kuwaandaa watu kufanya mapinduzi".
Serikali ya mseto imesisitiza kwamba ni Tume ya uchaguzi peke yake ndio inaweza kutangaza matokeo ya uchaguzi.
Kanisa Katoliki, ambalo lina ushawishi mkubwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, limesema kuwa kuna mshindi wazi wa urais katika uchaguzi uliofanyika Jumapili, kwa mujibu wa matokeo ambao wamefanikiwa kuyaona.
Maaskofu wa kanisa hilo wamewataka watawala nchini humo kuwa wakweli na kutangaza matokeo hayo karibuni.
Kanisa hilo lina maelfu ya wangalizi wa uchaguzi nchini humo na baadhi wamewasilisha ripoti za dosari kadha wa kadha.
Bishops at a press conference
Image captionKanisa Katoliki limesema linafahamu nani alishinda uchaguzi, lakini halijataja jina lake
Tume ya uchaguzi ilitarajiwa kutangaza matokeo Jumapili lakini wiki hii ilidokeza kuwa huenda ikachelewa kufanya hivyo kwani bado haijapokea matokeo kutoka vituo vingi vya kupigia kura nchini humo.
Mkuu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (CENI) Corneille Nangaa alisema matokeo zaidi ya asilimia 80 ya kura bado yanasubiriwa.
Upinzani pia umelalamikia dosari kwenye uchaguzi huo.
Rais Joseph Kabila anatarajiwa kuondoka madarakani baada ya kuongoza kwa miaka 17 na ameahidi kukabidhi madaraka kwa atakayeshinda uchaguzi.
Man looking at voting materialHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMaafisa bado wanahesabu na kutathmini matokeo ya uchaguzi huo wa Jumapili
Baraza la Taifa la Maaskofu Congo (Cenco) halikusema nani linaamini alishinda uchaguzi huo.
Kanisa hilo limekuwa likipinga kuongezwa kwa muda wa Rais Kabila madarakani, tangu uchaguzi ulipoahirishwa mara kadha.

Wagombea wakuu wa urais DR Congo

Bw Kabila awali alitarajiwa kuondoka madarakani 2016 lakini uchaguzi ukaahirishwa kutokana na kile serikali ilisema ni kutokamilika kwa maandalizi.

Mtandao na TV

Huku matokeo yakisubiriwa, serikali imefungia matangazo ya runinga inayomilikiwa na mwanasiasa wa upinzani.
Msemaji wa upinzani Lambert Mende aliituhumu Canal Congo kwa kutangaza matokeo ya uchaguzi kabla ya matangazo rasmi kutolewa.
Hatua hiyo imejiri siku chache baada ya huduma ya mtandao wa intaneti kuzimwa taifa lote.
Canal Congo inamilikiwa na mbabe wa kivita wa zamani Jean Pierre-Bemba.
A staff of the Independent Electoral Commission (CENI) configures a voting machine on December 20, 2018Haki miliki ya pichaAFP
Image captionMashine za kielektroniki zilitumiwa katika shughuli ya kupiga kura kwa mara ya kwanza
Alizuiwa kuwania kutokana na kupatikana na hatia ya kuwahonga mashahidi katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) wakati wa kesi yake ya uhalifu wa kivita.
Anamuunga mkono mfanyabiashara Martin Fayulu.
Pamoja na kuifungia Canal Congo, seriali pia imefungia matangazo ya Radio France Internationale (RFI) na kufuta kibali cha mmoja wa waandishi wake, Florence Morice, wakimtuhumu kwa kuvunja sheria za uchaguzi.
Waangalizi wa uchaguzi wa Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika wameeleza uchaguzi huo wa Jumapili kama ulioendeshwa vyema.
Presentational grey line
Wagombea wa upinzani Martin Fayulu (kushoto) na Felix Tshisekedi (kulia) watakabiliana na Emmanuel Shadary (katikati ), aliyekuwa waziri wa maswala ya ndani.Haki miliki ya pichaAFP/REUTERS
Image captionWagombea wa upinzani Martin Fayulu (kushoto) na Felix Tshisekedi (kulia) watakabiliana na Emmanuel Shadary (katikati ), aliyekuwa waziri wa maswala ya ndani.
Nani waliwania?
Kulikuwa na wagombea 21 lakini watatu ndio wakuu:
  • Emmanuel Ramazani Shadary, Waziri wa zamani wa mambo ya ndani na mtiifu kwa Kabila, ambaye aliwekewa vikwazo na Muungano wa Ulaya kwa hatua zilizochuliwa upinzani wakati wa maandamano ya mwaka 2017.
  • Martin Fayulu, Mkurugenzi mkuu wa zamani wa mafuta ambaye ameahidi nchi yenye mafanikio lakini ambaye watu maskini wanahisi hawezi kuwatetea.
  • Felix Tshisekedi Tshilombo, Mtoto wa mwanasiasa mkongwe ambaye ameahidi kupambana na umaskini.

Comments

Popular posts from this blog

Wanakijiji watishia kumburuza kortini DC

TMA yatoa tahadhari mafuriko yaja