Magufuli ataka jina libadilishwe


Alhamisi , 20th Dec , 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli ameitaka mamlaka inayosimamia ujenzi wa wa Daraja la Selander kubadilisha jina hilo na kutoliita kwa jina la mtu, badala yake wanapaswa kubuni jina ambalo litaitangaza Tanzania.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli
Akizungumza katika uzinduzi wa uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa daraja hilo, Dk. Magufuli amesema kwamba jina la daraja hilo linapaswa kutangaza nchi haswa ikizingatiwa kuwa daraja hilo lipo maeneo ya ubalozi wa mataifa mbalimbali hivyo itakuwa rahisi kwao kusafiri kwa haraka.
"Hili jina la daraja 'New Selander Bridge', nafikiri mngelibadilisha na kuliita jina lingine ambalo litaitangaza Tanzania vizuri kimataifa. Hata mngeliita Tanzanite, kwani ni madini pekee yanayopatikana Tanzania ila msiite jina la mtu".
Pamoja na hayo Rais Magufuli ameongeza kwamba "Mwalimu Nyerere alikuwa na mawazo na maono mazuri, hata daraja la Nyerere yalikuwa ni mawazo yake ndio maana lilipokalimilika nilipendekeza liitwe jina lake, daraja hili pia yalikuwa ni maono yake naagiza lisiitwe jina la mtu".
Mbali na hayo Rais Magufuli amewasisitiza wakandarasi wa ujenzi wa daraja hilo kuhakikisha wanaimaliza kazi hiyo mapema kwa kuwa hakuna sababu inayoweza kuchelewesha na kwamba kama ni fedha zipo.

Comments

Popular posts from this blog

Wanakijiji watishia kumburuza kortini DC

TMA yatoa tahadhari mafuriko yaja