SARAH MOSES -DODOMA KAMBI ya Upinzani Bungeni, imemtaka Spika wa Bunge, Job Ndugai, kutengua uamuzi wake wa kusimamisha vikao vya kamati za Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa ( LAAC ). Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma jana, Mwakilishi wa Kambi ya Upinzani, John Mnyika alisema kauli aliyoitoa spika siyo ya Bunge, bali ni yake binafsi. “Haiwezekani mgogoro wa Spika na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Musa Assad, ukasimamisha mambo mengine ya bunge kuendelea. “Kama kamati tunamtaka spika abadilishe uamuzi wake kwa kamati hizi mbili na awezeshe kamati hizo kukutana kabla ya tarehe 25 mwezi huu,”alisema Mnyika na kuongeza: “Tumesikia spika amesimamisha kamati hizo kwa kuwa CAG ameitwa kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Januari 21, mwaka huu kwa kile alichokiita mgogoro wa CAG na Bunge … kauli hiyo siyo ya Bunge ila ni yake binafsi”. Alisema uamuzi alioutangaza Spika
Comments