Pigo kubwa upinzani sherehe za krismas na mwaka mya

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko wamewatakiwa wanachama wao heri ya Sikukuu ya Krismasi na Mwaka mpya huku wakirudishwa rumande.

Wawili hao wametoa heri hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mara baada ya kuahirishwa kwa kesi yao ya uchochezi inayowakabili na viongozi wengine saba wa chama hicho. Wakili wa Serikali, Wankyo Simon, amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu.

Wilbard Mashauri kuwa kesi imekuja kwa ajili ya kutajwa. Wakili Simon amedai kuwa hawana taarifa ya kinachoendelea Mahakama ya juu hivyo wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa. Hata hivyo, Wakili Faraja Mangula alidai kuwa Wakili wa washitakiwa hao.

Peter Kibatala na Sheck Mfinanga wamepata dharura hivyo wanaomba mahakama ipange Januari 4, mwakani. Akijibu hoja hiyo, Wakili Simon amedai wanaiachia Mahakama ipange tarehe itakayoona inafaa. Hakimu Mashauri amesema Januari 4, mwakani atakuwa na kazi nyingine hivyo aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 3, 2019.

Baada ya kuelezwa hayo, Mbowe na Matiko waliwakia wafuasi wao heri ya sikukuu wakiamini kuwa hawawezi kutoka gerezani kwa kipindi hiki.

Washitakiwa wengine ni Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Katibu wa Chadema, Dk. Vincent Mashinji, Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya na Katibu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu.

Wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya February Mosi na 16, mwaka huu maeneo ya Dar es Salaam.

Comments

Popular posts from this blog

Kitakachojiri katika mabasi Des. 20

DRC CONGO :UN YAVIMBIWA