Wolper aogopeshwa



 Muigizaji wa filamu nchini Tanzania, Jacquiline Wolper amefunguka juu ya kuweka wazi mahusiano yake kwenye mitandao ya kijamii.

Wolper katika mahojiano yake na Dizzim Online, amesema kuwa ukiwa unaposti mtu ambaye uko nae kimapenzi inakuwa rahisi wabaya wako kumuiba hasa mtu akiwa na makalio makubwa.

"Unajua kitu kimoja tunshindwa kuelewa wadada ambao tulikuwa tuna expose mapenzi yetu kuna mtu tu ana matamanio yake anachuki na wewe anaona aah huyu Wolper anatupostia bwana ake sasa na mimi na hili kalio langu ngoja nikamchukue yule bwana sijui unanielewa hana mapenzi na bwana ako anakuja tu kukukomesha kwahiyo upostiji wako, " amesema Wolper.

"Unafanya wale wa baya wako watafute pa kukuumiza, Wale wanaonyakuliwa hawajui kwamba nimependwa na nimetakiwa kwaajili yako kwasababu wao wana watu wao hawataki kuwa expose."

Comments

Popular posts from this blog

Wanakijiji watishia kumburuza kortini DC

TMA yatoa tahadhari mafuriko yaja