Rais azitafuta fedha zilizojenga nyumba hewa
Ijumaa , 21st Dec , 2018 Na Mwandishi wetu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Maguful, amebainisha sababu za kufanya mabadiliko kwenye Jeshi la Magereza kuwa ni kutokana kutoa fedha ambazo aliagiza kujengwa kwa nyumba za maaskari lakini mpaka sasa hazijajengwa. Rais Magufuli Rais Magufuli ametoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam wakati akizungumza kwenye hafla ya utoaji vyeo kwa wahitimu wa maofisa na Ukaguzi, ambapo ameshangazwa kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya askari magereza lakini hakuna iliyojengwa. " Kule Magereza nilitoa pesa kwa ajili ya kujenga nyumba za askari magereza pale Ukonga, zile nyumba mpaka leo hazipo na hela zimeisha, ndiyo maana nilifanya mabadiliko haraka haraka pale ". " Niwaeleze ukweli huwa ninauvumilivu lakini uvumilivu wa kwenye fedha huwa unanishinda, unatoa nyumba kwa ajili ya maaskari lakini hakuna kinachojengwa, nimemuagiza Kamishna Magereza azifuatilie h...



























Comments